Tuesday, 19 January 2016

WABUNGE UINGEREZA WAMJADILI TRUMP

Donald Trump ametaka waislamu kupigwa marufuku kuingia nchini Marekani Wabunge wa Uingereza wamekuwa na mjadala kuhusu kupigwa marufuku au la kwa anayewania nafasi ya kupeperusha bendera ya chama cha republican katika kinyang'anyiro cha urais wa Marekani, Donald Trump kuingia nchini Uingereza.
Mjadala huo uliochukua muda wa saa tatu umekuja baada ya karibu nusu milioni ya watu nchini Uingereza kuunga mkono hatua ya kumzuia Trump kuingia Uingereza. baada ya Trump kusema kuwa Waislamu wote wazuiwe kuingia marekani ikiwa ni njia ya kupambana na vitendo vya kigaidi
Wabunge hata hivyo hawakuonyesha shauku kubwa ya kumfungia milango Trump ili asiingie Uingereza kwani hakuna kura yeyote iliyopigwa mwishoni mwa mjadala
Mmoja wa wabunge wa Uingereza ambaye ni muislamu amesema kauli za Trump ni sumu, huku msemaji wa idara ya mambo ya ndani Jack Dromey akisema kuwa Trump azuiwe kuingia Uingereza.
Trump atumia wito kuhusu Waislamu tangazoni Cruz mbele ya Trump utafiti wa maoni Iowa
Wakati huo huo Trump ameendelea na kampeni zake, akizungumza katika chuo cha Liberty, chuo binafsi cha kikristo kilicho Lynchburg, Virginia amewaambia wanafunzi wa kikristo kuwa wanapaswa kuungana kuilinda dini yao.
''Tunapaswa kuilinda kwa kuwa kuna mambo yanafanyika, mambo mabaya sana, sijui ni nini lakini hatuungani labda.dini nyingine wanaungana kuzuia, hapa tunayo...ukitazama nchi hii, asilimia 70 mpaka 75 ni wakristo, watu wengine wanasema hata zaidi ya hiyo, inadhihirisha nguvu tuliyonayo, tunapaswa kuungana'' alieleza Trump katika kampeni yake.BBC

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA