MHANDISI SULEIMAN SAID AZIKWA MAKABURI YA KISUTU
Dua
maalum ya mazishi wakati wa safari ya mwisho ya aliyekuwa Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), marehemu Mhandisi Suleiman
Said, katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam. (Picha zote na
Andrew Chale, Modewjiblog).
Safari ya
mwisho ya mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege (TAA), Mhandisi Suleiman Said, imehitimishwa katika makaburi ya
Kisutu majira ya saa 10 jioni jana huku watu mbalimbali wakijotokeza
kwa wingi katika mazishi hayo.
Mbali na
ndugu jamaa na marafiki, viongozi wa Serikali, vyama pamoja na wadau wa
michezo walikuwa miongoni mwa waliojitokeza katika makaburi hayo ya
Kisutu yaliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Marehemu
Mhandisi Suleiman Said alipatwa na umati huo mapema jana asubuhi 18
Januari akiwa katika mazoezi ya kuogelea na ndipo kuzidiwa na baadae
kukimbizwa hospitali ya The Agha Khan na kufikiwa na umati wake huo.
Marehemu
pia atakumbukwa kwa wadau wa michezo hasa klabu ya Simba Sc ambayo
aliwahi kuwa Katibu Mkuu kipindi cha nyuma huku akiwa mwanachama mwenye
mguso na msukumo mkubwa katika timu hiyo.
Hata
hivyo ndugu wa familia kupitia kwa msemaji wa familia makaburini hapo
wameeleza kuwa, taratibu zingine zitaendelea kwa familia ikiwemo dua
maalumu inayotarajiwa kusoma leo.
Umati wa ndugu, jamaa na marafiki waliojitokeza katika mazishi hayo..
Ndugu na jamaa wakisalimiana muda mfupi baada ya mazishi hayo..
Ndugu, jamaa na marafiki wakishiriki kuweka udongo na majani katika safari ya mwisho ya marehemu.
-mtandao
0 comments:
Post a Comment