ASKARI WALIOFARIKI KATIKA MSAFARA WA RAIS MAGUFULI WAAGWA SINGIDA
Askari
watatu wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, waliofariki dunia wakiwa
kwenye msafara wa rais Dkt. John Pombe Magufuli baada ya gari lao
walilokuwa wakisafiria kupasuka tairi la nyuma na dereva kushindwa
kulimudu wakitokea Singida kuelekea Dodoma wameagwa jana. Zifuatazo ni
picha za tukio hilo la kuaga miili ya askari hao.
Kamanda
wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP Thobias Sedoyeka, akitoa salamu
za pole kutoka kwa Mkuu wa jeshi la polisi nchini, Ernest Mangu na
polisi mkoa wa Singida kwa familia za askari polisi watatu waliofariki
dunia wakati wakiwa kwenye msafara wa rais Dk.Magufuli jana kutoka
Singida Dodoma.
Kamanda
wa Jeshi la polisi mkoa wa Manyara, ACP Camilius Wambura, akitoa salamu
za pole kwa familia na jeshi la polisi mkoa wa Singida, kwa kufiwa na
askari polisi watatu waliokuwa kwenye msafara wa rais Dk.Magufuli
wakitokea Singida kuelekea Dodoma juzi.
Mkuu wa
mkoa wa Singida,D k.Parseko Kone, akitoa salamu za pole kwa familia na
jeshi la polisi mkoa wa Singida, kwa kufiwa na askari 3 kwenye ajali
iliyotokea Isuna kwenye msafara wa rais Dk.Magufuli uliokuwa ukitokea
Singida kuelekea Dodoma juzi.
Askari
polisi mkoa wa Singida,wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa
Insp.Miraji mwigelo Kindamba,Insp.Kindamba ni moja kati ya askari 3
waliofariki juzi kwenye ajali iliyotokewa kwenye msafara wa Dk. Magufuli
uliokuwa ukitokea Singida kwenda Dodoma.
Baadhi ya
mamia ya waombolezaji wa msiba mkubwa wa askari polisi watatu
waliofariki juzi wakiongoza msafara wa rais Dk.Magufuli kutoka Singida
kwenda Dodoma.(Picha zote na Nathaniel Limu).
0 comments:
Post a Comment