Thursday 25 February 2016

Donald Trump ashinda Nevada

Donald-Trump
Mgombea wa urais wa Chama cha Republican, Donald Trump ameshinda katika Jimbo la Nevada nchini Marekani, na kuzidi kuimarisha uongozi wake katika mchujo wa kuwania tiketi ya chama hicho.
Tajiri huyo sasa ameshinda mara tatu, kufuatia ushindi wake katika Jimbo la New Hampshire na Carolina Kusini.
Seneta Marco Rubio na Ted Cruz ambao wamekuwa wakishambuliana wiki hii wanapigania nafasi ya pili.
Maofisa wa chama hicho wamesema wamekuwa wakichunguza ripoti za watu kupiga kura mara mbili huku eneo moja likidaiwa kuwa na vifaa vichache vya kupigia kura.
Baadhi ya watu waliojitolea pia walidaiwa kuvaa nguo zenye picha za bwana Trump, lakini maofisa wamesema kuwa hatua hiyo siyo kinyume na sheria. 
BBC

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA