KATIBU WA CWT MANISPAA YA IRINGA AMETANGAZA MGOGORO NA MKURUNGEZI WA MANISPAA YA IRINGA
katibu wa cha walimu manispaa ya iringa mwalimu Fortunate Njalali akiwa ofisini kwake
siku kadhaa zimepita toka kufanyike uzinduzi wa baraza la wafanyakazi la manispaa ya iringa kwa ajiri ya kujadili baadhi ya agenda za kulijenga upya baraza hilo,lakini chama cha walimu manispaa ya iringa kimegoma kuhudhuria baraza hilo kutokana na kukiuka baadhi ya vipengele vya makubaliano ya awali.
Akizungumza na blog hii katibu
wa cha walimu manispaa ya iringa mwalimu Fortunate Njalali amesema kuwa sababu
ya kugoma kuingia kwenye baraza la
halmashauri ya manispaa ya iringa kwa kuwa baraza hilo limepitwa na muda hivyo
kunaitajika kuliunda baraza jimpya ndio waweze kuingia kwenye baraza la
wafanyakazi.
Aidha katibu Njalali amesema
kuwa wamekuwa wakiingia kwenye baraza la wafanyakazi kinyume cha sheria kwa
majadiliano maalumu hivyo walikuwa wakihudhuria baraza batili na walikuwa
wakimuambia mkurungezi juu ya swala hilo.
Njalali amesema kuwa
haiwezekani baraza la wafanyakazi likawa na viongozi wengi kuliko wafanyakazi
wenyewe hivyo watakuwa hawawatendei haki kwa kuwa hawatakuwa na hoja za msingi
zinazowahusu wafanyakazi wenyewe.
“Angalia humu kwenye baraza
hili tumejaa viongozi tu watumishe au walimu wenyewe wanawakilishwa na nani na
tutengemee matokeo gani kwa miaka ya baadae kwa kupitisha bajeti isiyokuwa na
mashiko kwa wahusika”.alisema Njalali
Njalali ameongeza kuwa
hawawezi kuingia kwenye baraza la wafanyakazi ambalo halina viongozi kwa kuwa
viongozi waliopo hawana uwezo wa kuwa viongozi wa kuongoza baraza hilo kutokana
na uwezo wao wa kitendaji.
“Hatuwezi kuongozwa na
wajumbe na viongozi haramu kwa kuwa wamekiuka sheria na wanaijua hilo na kama mkurugenzi atandesha
baraza hilo basi baraza hilo litakuwa batili kwa kuwa chama cha walimu ndio
waliosaini mkataba huo”.alisema Njalali
Lakini Njalalia ametangaza
rasmi mgogoro na mkurungezi wa manispaa ya iringa kwa kukiuka makubaliona
waliokubaliana hapo awali wakati wa kusaini mkataba na kuwahidi walimu kuwa
watampeleka mkurugezi CMA
“Nimemwandikia barua kuwa
nimetangaza mgogoro na mkurugezi na nimempa siku tano kukutana na viongozi wa
chama cha walimu manispaa ya iringa vinginevyo tarehe kumi na sita mwezi huu
nampeleka kwenye baraza la usuruhishi CMA kwa kukiuka sheria na makubailiona ya
mkataba wetu”.alisema Njalali
Njalali alimalizia kwa
kusema kuwa baraza la wafanyakazi linafaida kwa watumishi kwa kuwa
wanajadiliana na muaji wao juu ya mazingira ya kazi yao na wafanya nini ili
kuboresha ufanyaji wa kazi zao na kuongeza ubunifu wa kuboresha kazi.
“Tumekuwa tunapitisha bajeti
nyingi lakini hakuna mrejesho wowote ule wa ile bajeti tunayoipitisha hivyo tumekuwa tunaburuzwa mara kwa mara kwa
sasa basi hatutaki kuburuzwa tena tunataka haki yetu na ndio maana tumetangaza
mgogoro na mkurugenzi wa manispaa ya iringa”alisema Njalali.
Tulipomtafuta mkurugezi wa
manispaa ya iringa hakupatika kujibia kero hii iliyotolewa na katibu wa
CWT,hata hivyo baraza la wafanyakazi lilifanyika na wakafanya uchaguzi wa
kuwachagua viongozi wapya wa baraza hilo.
0 comments:
Post a Comment