PAPA FRANCIS: DONALD TRUMP 'SI MKRISTO'
Papa Francis asema Donald Trump si mkristo
Mkuu wa
kanisa katoliki duniani Papa Francis amesema kuwa wazo la mgombea wa
kiti wa chama cha Republican nchini Marekani , Donald Trump la kujenga
ukuta kati ya Mexico na Marekani si ukristo.
Papa
Francis alisema kuwa kwa mtu yeyote ambaye katika karne hii ya 21
anayetaka kujenga ukuta badala ya kujenga daraja huyo si mkristo
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki aliyasema hayo katika siku yake ya mwisho ya ziara nchini Mexico.
Trump
ambaye anapigiwa upatu kutwaa tikiti ya chama cha Republicans katika
uchaguzi mkuu ujao amependekeza kujenga ukuta na ua katika mpaka kati ya
nchi yake na mexico ilikuwazuia wahamiaji kuingia nchini Marekani.
Trump amesema kuwa papa Francis hana haki yeyote kumhukumu iwapo ni muumini au la
Licha ya
kuwaambia waumini wa kanisa Katoliki kuwa hatawazuia kutumia uhuru wao
kumchagua rais wanaompenda, papa Francis amesema kuwa iwapo Trump
anapanga kujega ua basi ''si mkristo''
Hilo haliambatani na mafunzo ya injili
"sharti tutathmini matamshi yake '' tunapaswa kuchunguza kwa kina ''
Bwenyenye
Donald Trump kwa upande wake amesema kuwa papa Francis hana haki yeyote
kumhukumu iwapo ni muumini au la ''inasikitisha'' alisema Trump.
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki aliyasema hayo katika siku yake ya mwisho ya ziara nchini Mexico.
Mtazamo
huo wa papa Francis bila shaka unatarajia kuwapa wapinzani wa Trump
fataki huku wakiendelea na kura za mchujo ambapo msimamo wa kidini wa
mgombea unatazamwa na wapiga kura wengi kuwa kigezo muhimu.
1 kati ya wamarekani 5 ni wakatoliki.
Papa Francis ni maarufu sana nchini Marekani.
-BBC
0 comments:
Post a Comment