TAMASHA LA PASAKA MWAKA HUU KUFANYIKA MACHI 28 WILAYANI KAHAMA
Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani), jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Tamasha la Pasaka litakalofanyika Mkoani Shinyanga Wilayani Kahama Machi 28 mwaka huu ambapo Tamasha la Pasaka mwaka huu halitafanyika jijini Dar es Salaam na baadala yake kufanyika mikoani.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama wakati akizungumza nao leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
TAMASHA la Pasaka mwaka huu kufanyika Machi 28 Mkoani Shinyanga katika viwanja kahama wilaya ya Kahama, ambapo tamasha hilo limewapa kipaumbele waimbaji wa ndani ya nchi yetu.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Msama amesema kuwa Kauli mbiu ya Tamasha la Pasaka mwaka huu ni "UMOJA NA UPENDO HUDUMISHA AMANI KATIKA NCHI YETU". ambayo itatawala katika tamasha hilo hapa nchini.
Msama amesema kuwa Mwimbaji wa nyimbo za Injiri Bonfasi Mwaitege amethibisha kutumbuiza katika tamasha hilo pamoja na Mwimbaji wa nyimbo za Injiri Rose Mhando.
Aidha Msama amelishukuru Balaza la Sanaa Tanzania(BASATA) kwa kuruhusu kufanyika Tamasha la Pasaka wilayani Kahama pia amewaomba wananchi wajitokeze kwa wingi katika tamasha hilo mkoani humo.
0 comments:
Post a Comment