Tuesday 8 March 2016

WAMERUDI:: YANGA YAICHABANGA AFRICAN SPORTS 5-0 NA KUREJEA KILELENI

yangaa
Klabu ya Yanga Wanajangwani leo Machi 8.2016 wamefanikiwa kurejea kileleni mwa ligi Kuu ya soka ya Tanzania Bara (VodaCom Premier Legue-VPL) kwa kuiangushia kipigo cha mabao 5-0 Wana Kimanumanu African Sports, mchezo uliomalizika dakika chache zilizopitakwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Wafungaji wa Yanga ni pamoja na Kelvin Yondani bao moja, Ngoma (1) Tambwe (1) Matheo (1).

Mchezo huo wa aina yake, Yanga ilijihakikishia ushindi mapema baada ya kupata mabao kuanzia kipindi cha kwanza tu cha mchezo na hadi kufikia kipindi cha pili walikwisha jifikishia mabao 5-0 dhidi ya wanakimanumanu hao.
Kwa ushindi huo, Yanga inarejea tena kileleni mwa ligi huku kwa kufikisha pointi 50 na kuwashusha watani zao Simba SC ambao walikuwa wanaongoza ligi hapo awali ambao sasa wamerudi hadi nafasi ya pili kwa kubakia na pointi zao 48 za awali, huku Azam wao wakibakia nafasi hiyo hiyo ya tatu kwa kuwa na pointi 47.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA