Thursday 26 May 2016

RAIS DKT.MAGUFULI AMTEUA ALIYEKUWA WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA KUWA MKUU WA CHUO KIKUU HURIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).

Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 25 Mei, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Mheshimiwa Pinda unaanza mara moja.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam

25 Mei, 2016

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA