ARSENAL YATAMBULISHA 'MIDO' MPYA GRANIT XHAKA KUTOKA BUNDESLIGA
Kiungo mpya wa Arsenal,Granit Xhaka akiwa amepozi na jezi ya timu hiyo baada ya kukamilisha usajili wa Pauni Milioni 35 kutoka Borussia Monchengladbach ya Ujerumani.
UHAMISHO
wa Granit Xhaka kutua Arsenal umeiva bada ya picha za mchezaji huyo akipozi kwa
ajili ya kupigwa picha kwenye uwanja wa mazoezi ya klabu hiyo wa London Colney
kuvuja. Kiungo huyo, 23, aliwasili London Ijumaa iliyopita kwa ajili ya
kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kusaini mkataba wa miaka minne na Arsenal na
picha za Xhaka akiwa ametinga jezi mpya za Arsenal zitakazovaliwa msimu ujao wa
2016/17, ambazo pia bado hazijatambulishwa rasmi.
Mchezaji
huyo wa kimataifa wa Uswisi amekuwa akifuatiliwa na Arsene Wenger kwa miezi
kadhaa na baada ya kuafikiwa kwa ada ya uhamisho ya pauni mil 33.3 na
klabu yake ya Borussia Monchengladbach, anakuwa mchezaji wa kwanza
kuwasili Arsenal katika kipindi hiki cha usajili kinachotarajiwa kuwa ‘bize’.
Mtumiaji wa ukurasa wa Twitter, Valon Demiri ambaye maskani yake ni Kosovo,
aliposti picha hizo kwenye mtandao wa kijamii baada ya kuripotiwa kuzipata
kutoka kwa mtu wa karibu na Xhaka.
Kiungo
huyo ametua London na wazazi wake, kaka yake na mkewe kwa ajili ya kufanyiwa
vipimo vya afya na kupozi kwa ajili ya picha kabla ya kutangazwa rasmi kwa
usajili huo.
0 comments:
Post a Comment