Tuesday 31 May 2016

TANGAZO MUHIMU:: JKT YABADILI TAREHE YA KURIPOTI KWA WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI HILO KWA MUJIBU WA SHERIA


TANGAZO

MABADILIKO YA TAREHE YA KURIPOTI KATIKA MAKAMBI YA JKT KWA VIJANA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2016.


Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linautangazia umma mabadiliko ya tarehe ya kuripoti makambini vijana wote waliohitimu kidato cha sita mwaka 2016 na kuchaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2016.


Taarifa ya awali kwa vyombo vya habari nchini ilianisha tarehe ya kuripoti kuwa ni tarehe 01 June hadi tarehe 05 Juni 2016. Tarehe hiyo imeafanyiwa mabadiliko badala yake vijana hao wanatakiwa kuripoti katika makambi ya JKT waliyopangiwa kuanzia tarehe 07 June hadi tarehe 10 June 2016 bila kukosa.


Atakayesikia tangazo hili amtaarifu na mwezie.




Kwa Taarifa Zaidi Tembelea  Tovuti http://www.jkt.go.tz/
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 31 Mei 2016

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA