KAMATI YA MAWASILIANO MKOA WA MWANZA YATOA ELIMU KWA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA MAWASILIANO
Mwenyekiti wa Kamati ya
Mawasiliano Mkoa wa Mwanza, Jonathan Abdallah Kasibu, akizungumza katika Semina
kwa Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Jijini Mwanza iliyofanyika jana katika
Ukumbi wa Shule ya Sekondari Mwanza.
Katika semina hiyo,
watumiaji wa hudumza za mawasiliano ikiwemo simu pamoja na vyombo vya habari
ambao waliwakilisha makundi mbalimbali kama vile wanahabari, wajasiriamali na
walemavu, walipewa elimu juu ya uwepo wa Kamati hiyo pamoja na uwepo wa Baraza
la Ushauri la Watumiaji wa huduma za Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano
nchini (TCRA-CCC).
Pia walielimishwa juu ya
mwongozo wa kuwasilisha malalamiko ya watumiaji wa huduma za mawasiliano, haki
na wajibu wa mtumiaji wa huduma za mawasiliano pamoja na sheria ya makosa ya
mitandao ya mwaka 2015.
Semina hiyo pia
ilihudhuriwa na viongozi wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za
Mawasiliano, kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA-CCC) ambapo iliambatana
na viongozi wa Kamati ya Mawasiliano mkoani Mwanza kujitambulisha kwa baraza
hilo.
Watumiaji wa huduma za
mawasiliano walielezwa kwamba ni wajibu wao kuwasilisha malalamiko yao ikiwa
wanapokea huduma zilizo chini ya kiwango ama ikiwa wana malalamiko ya aina
yoyote kuhusu huduma za mawasiliano.
Walihimizwa kuwasilisha
malalamiko yao kwa kuanza na mtoa huduma, yasiposhughulikiwa wanawayawasilisha
katika Kamati ya Huduma za Mawasiliano mkoa, yasipotatuliwa yatawasilishwa katika
Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano kutoka TCRA na hata
ngazi nyingine zaidi hadi pale utatuzi utakapofanyika.
Semina hiyo ilionekana
kuwafungua ufahamu watumiaji wa huduma za mawasiliano jijini Mwanza kwani
baadhi yao walieleza kuwa awali walikuwa hawatambui haki na wajibu wao katika
kutumia huduma za mawasiliano.
Baadhi ya
Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Jijini Mwanza, wakiwa katika semina ya
kuwaelimisha juu ya Matumizi ya Huduma za Mawasiliano.
0 comments:
Post a Comment