WAKULIMA WA ZAO LA SHAYIRI WANAOSHIRIKIANA NA TBL GROUP WAADHIMISHA SIKU YAO
Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha akihutubia wananchi
Wakulima wa Shayiri wakitembeza wageni mashambani
Wakulima wa zao la Shayiri kanda ya Kaskazini mwa Tanzania wanaoshirikiana na kampuni ya TBL Group wameadhimisha siku yao wilayani Karatu ambapo mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha wakiwemo wadau wao kutoka SABMiller,na makampuni mengine yanayouza madawa na pembejeo za kilimo.
Wakulima waliweza kufanya maonyesho mbalimbali ya kazi zao pia walielezea mafanikio walioweza kuyapata kutokana na kilimo cha zao la Shayiri
Maofisa wa SABMiller na wafanyakazi wa TBL wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho hayo ambapo pia TBL Group ilitunukiwa tuzo kwa kendeleza kilimo cha zao la Shayiri nchini
Mkuu wa Uendelezaji Kilimo cha Shahiri wa SABMiller kanda ya Afrika Thinus Van Schoor akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wakulima wa Shayiri
Naibu Waziri wa Kilimo,Chakula na Maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha (kulia) akimpongeza mkulima aliyejishindia zawadi ya kabati
Naibu Waziri wa Kilimo,Chakula na Maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha (kushoto) akimpongeza mkulima wa Shayiri kutoka Kijiji cha Lendikinya wilaya ya Monduli,Masiaya Oloshuda aliyeshinda kwenye bahati nasibu ya kupata vifaa vya usalama shambani
0 comments:
Post a Comment