MAHAKAMA KUU KANDA YA TANGA YATUPILIA MBALI SHAURI LA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI JIMBO LA PANGANI
Mbunge
wa Jimbo la Pangani (CCM)Jumaa Aweso wa pili kutoka kulia akiwa na
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini,Stephen Ngonyani "Proffesa Maji
Marefu " wakiwa ndani ya
Mahakama Kuu Kanda ya Tanga wakisuburia kuanzwa kwa kesi hiyo hata hivyo
hukumu hiyo ilimpa ushindi halali Mbunge Aweso katika Uchaguzi Mkuu
uliofanyika Octoba mwaka jana mara
baada ya kuonekana hakuna vigezo vya kutengua matokeo hayo katika kesi
ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CUF Amina
Mwidau
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tanga jana
imetupilia mbali shauri la kupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la Pangani
lililofunguliwa na aliyekuwa mgombea kupitia tiketi ya CUF Amina
Mwindau dhidi ya Mbunge wa Jimbo hilo Jumaa Hamidu Aweso CCM na
kuonekana hakuna vigezo vya kutengua matokeo hayo.
Akizungumza wakati akitoa huduma ya Shauri hilo,Jaji Patricia Fikirini
alisema mlalamikaji Amina Mwindau CUF ameonekana kushindwa katika shauri
hilo dhidi ya mlalamikiwa Jumaa Aweso katika upingaji wa matokeo ya
uchaguzi mkuu uliofanyika oct 25 mwaka jana.
Alisema miongoni mwa malalamiko yalioambatanishwa kutoka kwa mlalamikaji katika zoezi zima la kupinga matokeo hayo ni pamoja na kuwa
mlalamikiwa ambae ni Jumaa Aweso katika kampeni zake alikiuka taratibu
za uchaguzi,ubaguzi wa mgombea wa jinsia ya kike na kutumia lugha ya
siziokuwa za kiungwana jambo ambalo mlalamikaji alidai lilimgharimu
kupata matokeo mazuri katika uchaguzi huo.
Alisema sambamba na vielelezo vilivyoletwa mahakamani hapo pamoja na
ushahidi uliotolewa kwa upande wa mlalamikaji havikuwa na ushawishi wa
kuweza kutengua matokeo ya uchaguzi huo.
Jaji Fikirini alisema amezingatia hoja zote kutoka pande mbili na kujiridhisha Jumaa Aweso ambae ni mbunge hivi sasa kuwa ni mbunge
aliyepita kihalali na hakukuwa na vigezo vya upingwaji wa matokeo
aliyopata katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Alisema haki zote za kisheria zipo wazi kwa pande zote mbili mlalamikiwa na mlalamikaji ikiwa pamoja na kukata rufaa kwa maamuzi
yaliyochukuliwa na Mahakam hiyo ikiwa kama kuna upande hauta ridhika na
hukumu iliyotolewa.
Kwa upande wake Wakili wa kujitegemea na mahakama kuu Warehema Kibaha
alisema Jaji Patisia Fikirini amefanya maamuzi sahihi ya kutenda haki
kwa mteja wake katika shauri hilo lililo dumu kwa takriban miezi
7.
Wakili Kibaha alisema katika shauri hilo walijiandaa kwa ushahidi na
mashahidi wazuri ili kuweza kukabiliana na kesi hiyo jambo
ambaloliliwawezesha kupata ushindi wa kihalali na kuweza kumpa nafasi
mteja
wake kuendelea na majukumu yake ya Kibunge.
Nae Wakili Mashaka Ngole aliyemsimamia Mlalamikaji Amina Mwindau alisema
hana pingamizi lolote na atamsikiliza mteja wake ikiwa ataamua kukata
rufaa wataangalia vigezo muhimu vitakavyo wasaidia katika awamu ya pili
pindi watakapo kata rufaa hiyo
Mbunge wa Jimbo la Pangani Jumaa Aweso ambaye alikuwa anakabiliwa katika
shauri hilo alisema kipindi chote alichokuwa anakabiliana na kesi hiyo
kulimpotezea umakinifu wa kufanya majukumu yake ya kibunge na kuweza
kuangalia shida za wananchi wa Pangani kwa umakini zaidi.
Aweso alisema kesi imekwisha na sasa kilichombele yake ni kupambana na
kero za wananchi wa Wilaya hiyo ili kuweza kuwaletea maendelo kama
alivyowaahidi kipindi cha kampeni.
0 comments:
Post a Comment