Tuesday 19 July 2016

SEHEMU YA TATU::NAMNA YA KUONDOA MSONGO WA MAWAZO NA MFADHAIKO

Dalili Za Kuwa Na Msongo Wa Mawazo

mfadhaiko uitwao pyschotic depression

  • Kupata usingizi kwa shida
  • Kuona kuwa kila wakati umezidiwa na shughuli
  • Kukosa kumbukumbu
  • Kukosa uwezo wa kutuliza akili kwenye jambo moja
  • Mabadiliko katika tabia yako ya kula
  • Kuwa na wasiwasi
  • Kusikia uchungu, hasira au kukata tamaa haraka
  • Kuona kuwa huwezi kufanikisha mambo yako katika maisha

Wasiwasi (Anxiety)

Matatizo yanayowapelekea watu kwa wingi kuwaona wataalamu wa tiba ya akili ni msongo wa mawazo (Stress), mfadhaiko (Depression)na wasiwasi (Anxiety).
Wasiwasi (Anxiety) ni hali ya kuwa na hofu kuwa kuna jambo kubwa na baya litatokea juu yako. Wasiwasi unaweza kuwa wa kwaida tu au ukalenga sehemu fulani, kikundi fulani cha watu au kitu fulani. Zifuatazo ni njia kadhaa zitakazokusaidia na kukufanya urejee katika hali yako ya kawaida.
1.Jenga Mahusiano Ya Kusaidiana:Kupata msaada ni jambo ambalo litakusaidia sana katika kuondoa wingu la mfadhaiko lililoko mbele yako, peke yako itakuwa vigumu kuendelea na jitihada zako za kupambana na tataizo hili. Mfadhaiko kwa tabia yake, utakuzuia kutoka na kwenda kuomba msaada kwa watu wengine, lakini elewa kuwa kujitenga na upweke vinachangia kuukuza mfadhaiko ulio nao.
2.Jichanganye kwenye shughuli: Mara nyingi utakapokuwa kwenye mfadhaiko utapenda kujitenga na kubaki peke yako, hali ikizidi kubaki palepale tofauti na pale utakapochinganya kwenye shughuli za kijamii ambapo mfadhaiko wako utapungua. Jitahidi kujichanganya hata kama hufurahishwi sana na shughuli hizo. Jaribu haya machache kwa kuanza kujenga mahusiano na watu:
3. Pambana Na Mawazo Hasi:Mfadhaiko hukufanya ukione kila kitu kuwa ni kibaya, wewe mwenyewe, mazingira unamoishi na mategemeo yako ya baadaye. Suluhu hapa ni kuyaondoa haya mawazo mabaya na kupandikiza badala yake mawazo mazuri.
4. Lea Mwili Wako Vizuri:Ili kuudhibiti mfadhaiko ni lazima uulee mwili wako, ikimaanisha kuwa na mtindo wa maisha unaofaa, kujua namna ya kuudhiti mafadhaiko, kujua viwango vinavyoweza kufikiwa na mwili wako na kuweka kwenye ratiba muda wa kuuburudisha mwili wako.
5.Hakikisha unapata usingizi wa kutosha: Mfadhaiko kwa kawaida huendana na matatizo ya usingizi, unaweza kulala kupita kiasi au ukakosa usingizi. Vyote ni vibaya kwako. Tafata njia za kupata usingizi kwa muda wa saa 8 kwa siku.
6.Pata muda wa kukaa nje kila siku: Kukosa mwanga wa jua kunaweza kuifanya hali yako ya kuwa na mfadhaiko kuongezeka. Fanya matembezi nje, pata kahawa yako nje, kaa katika bustani n.k. Lenga kupata angalau dakika 15 za kukaa juani kila siku
7.Fanya Mazoezi Kila Wakati:Unapokuwa na mfadhaiko, mazoezi ni kitu cha mwisho ambacho mwili utapenda kufanya, lakini mazoezi ni kitu chenye nguvu sana katika kuondoa mfadhaiko. Utafiti umeonyesha kuwa mazoezi yana nguvu sawa na dawa za kuondoa mawazo. Sababu kamili haijaeleweka, lakini fikra moja ni kwamba mazoezi yanawezesha uzalishaji wa seli mpya katika ubongo.
8. Kula Chakula Kizuri:Chakula unachokula kina uhusiano na namna utakavyojisikia kimwili. Hakikisha unapata mlo kamili wenye protini isiyo na mafuta sana, chakula chenye wanga, matunda na mboga. Punguza matumizi ya kahawa, pombe na chakula kilichosindikwa kwa kemikali.
9. Usiruke milo: Kukaa muda mrefu bila kupata kitu cho chote kunaweza kukufanya ukose raha na kuwa mchovu, jaribu kula kitu fulani kila baada ya saa 3 au 4.
10.Punguza sukari na chakula kilichokobolewa: Chakula chenye sukari kwa wingi, kama vile vitu vidogo vidogo vya kutafuna (snacks) na pasta, vinaburudisha kwa muda mfupi lakini baadaye vinakusababishia kuingia kwenye hali ya fikra na kukupunguzia nguvu za mwili.
Nimatumaini yangu kuwa kwa haya machache utakuwa umesaidika kwa namna moja ama nyingine. Usisite kututumia maoni yako.
MWISHO
Kama ulikosa sehemu zilizopita bofya hapa kwa >>SEHEMU YA KWANZA <<
                                                                                                     >>SEHEMU YA PILI<<
-KDMULA

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA