Friday 25 November 2016

DKT. MPANGO:HALI YA UCHUMI TANZANIA NI NZURI


  Waziri wa fedha na mipango Philip Mpango akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa 18 wa taasisi za fedha
  Gavana wa Bank kuu Benno Ndulu akiongea na waandishi wa habari Na 
Woinde Shizza,Arusha 

PAMOJA na mtikisiko wa uchumi nchini Waziri wa fedha na mipango Philip Mpango amejitokeza na kusema hali ya uchumi Tanzania ni nzuri. 

Aliyasema hayo leo jijini Arusha wakati akifungua mkutano wa 18 wa taasisi za fedha nchini ulioandaliwa na BOT Arusha wenye lengo la kuzungumzia namna ya kutumia fursa za kijografia katika kukuza uchumi. 

Mpango alisema hali ya uchumi siyo mbaya bali watu ndio hawataki kufanya kazi na waliozoea kupiga dili nyepesi ndio wanalalamika ila serikali haina tatizo hilo. 

" Hata kama liwe taifa gani halikosi changamoto hivyo na sisi ni jambo la kawaida hata watu wa uchumi wanazidi kupima bado taifa letu haliko vibaya" Alisema . 

" hali ya uchumi inaenda vizuri tukiangalia sekta za fedha, deni la taifa, na hali ya chakula ipo vizuri tufanye kazi waliozoea dili nyepesi ndo wanaolalamika " aliongeza. 

Aliagiza taasisi za fedha nchini kukopesha katika sekta za Kilimo ili kuchochea sekta hiyo kufanya vizuri. 


Alisema pia ni vyema wakulima wakapatiwa elimu pamoja na mikopo yenye riba nafuu ili sekta hiyo iweze kuzalisha zaidi. 

Alisema awali serikali ilitoa maagizo kwa taasisi hizo kuhakikisha wanaiangalia sekta ya kilimo kwa ukaribu katika mikopo ili iweze kuzalisha na nchi iwe na maendeleo kupitia sekta hiyo. 

Naye Gavana wa Bank kuu Benno Ndulu Alisema lengo la mkutano huo ni kuzungumzia jinsi gani taasisi za kifedha zitatumia fursa za jografia kuhakikisha uchumi unapanda. 

Alisema changamoto inayosababisha washindwe kukopesha sekta ya kilimo ni kutolipwa fedha zao kwa wakati na wakulima hivyo wanahofia kuwakopesha. 

" Tatizo linalofanya tushindwe kukopesha ni kutokana navigezo vya watu Kushindwa kurejesha mikopo" alisema Ndulu. 

Hata hivyo alisema watawapatia elimu na kuwaweka karibu ili wawapatie mikopo hiyo. 

Sambamba na hayo Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dkt. Charles Kimei alisema wanaunga mkono kauli ya Serikali ya kutaka kuelekeza nguvu kubwa ya mikopo katika sekta ya kilimo na wapo tayari kuifanyia kazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dkt. Charles Kimei akitoa hutuba katika mkutano huo

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA