WAKAKA HII INAWAHUSU:: HAYA NDIO MAMBO YA MUHIMU PALE MNAPOANZA MAHUSIANO NA MSICHANA UMPENDAE

Nini cha kufanya baada ya kukubaliwa kuwa wapenzi?
Kama sio mpitaji kwake, na unataka uhusiano wenu uwe ‘Serious’, usikurupuke kuanza kumuomba kukutana nae katika sehemu ambazo zinatoa picha ya wazi kuwa unatengeneza mazingira ya kufanya nae ngono. Jitahidi kumfanya aone unamhitaji yeye na sio ngono.
Kumbuka katika kipindi hiki, kama ni mwanamke mwenye akili na anaetaka uhusiano ‘serious’ kila unachofanya au unachoongea kwake kina maana kubwa na anakuchorea picha ya maisha yenu ya baadae katika ubongo wake.
Kuwa mvumilivu, tengeneza uhusiano wa kwanza kama urafiki uliopitiliza na muoneshe kujali na kumpenda sana kisha mengine yatatiririka kwenye mkondo huo hadi mtakapoanza maisha ya Uchumba na kufikia hatua ya Ndoa.
Usimpoteze mkeo mtarajiwa kwa kuonesha kiu ya ngono zaidi ya kiu ya kuwa naye kama mpenzi unaetaka kufanya nae maisha.
Angalizo: Kwa bahati mbaya, baadhi ya wanaume hutumia mbinu hii kufanya maigizo ya kumnasa msichana ambaye kiuhalisia unaweza kukuta anamhitaji kwa ajili ya ‘Ngono’ tu lakini antigiza yote hata miaka kadhaa ili kumnasa.
Matokeo yake mapenzi haya huwa shubiri baada ya muda mfupi na
kumuacha msichana aliyenasa bila kujua akiwa na majonzi makubwa. Huu ni ukatili
wa kisaikolojia ambao mwanaume yeyote lijari anapaswa kuufikiria kwa kuwa
unaweza kugeuka kuwa ugonjwa utakaomtesa mwenzi wake na hata kupelekea kuwaza
kujiua.
Ili kuepuka athari kubwa ambayo unawez kuisababisha, ni vyema ukausikiliza kwanza moyo wako kama unataka kuingia kweli kwenye uhusiano serious na msichana kabla ya kufanya hivyo. Kumbuka mapenzi ni uwanja mpana zaidi ya ngono. Kuwa mkweli tangu unapoanza mahusiano.
Usikurupuke na usione aibu kujitoa pale unapoona unapotea lakini pia usiingie ili kumridhisha mtu kumbuka haya maisha ni yako na mwisho utatoa hesabu ya kila neno na tendo.
-Kd mula
0 comments:
Post a Comment