MESSI ABADILI NIA SASA KUITUMIKIA TIMU YA TAIFA
Nyota wa Argentina Lionel Messi ametengua uamuzi wake wa kustaafu kuchezea timu yake ya taifa na ni dhahiri sasa atalitumikia taifa lake ikiwa ni mwezi mmoja tangu atangaze uamuzi huo kufuatia kushindwa kutwaa ubingwa katika michuano ya Copa America 2016 iliyofanyika nchini Marekani.
Vyombo vya habari nchini Argentina vimeripoti kuwa vimemkariri Messi amegeuza nia kwaajili ya mapenzi aliyonayo kwa nchi yake naTayari kocha mpya Edgardo Bauza amemjumuisha nahodha huyo katika kikosi cha timu hiyo
"Tunahitaji kurekebisha mambo mengi katika soka la Argentina , lakini mimi nimependelea kufanya hivyo kutoka ndani na si kukosoa kutoka nje"alisema Messi
0 comments:
Post a Comment