Wednesday 14 September 2016

PROF. MBARAWA ATOA MIEZI SITA KUMALIZA UPANUZI WA UWANJA WA NDEGE WA MWANZA

ra1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mkandarasi Nyanza Road Construction inayojenga barabara ya Furahisha hadi Pasiansi KM 2.8 wakati alipokagua ujenzi wa barabara hiyo, jijini Mwanza.
ra2
Mkandarasi wa kampuni ya Nyanza Road Construction inayojenga barabara ya Furahisha hadi Pasiansi akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipokagua ujenzi wa barabara hiyo jijini Mwanza. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka Mkandarasi wa kampuni…. ya anayejenga uwanja wa ndege wa Mwanza kumaliza kazi ya upanuzi wa uwanja huo ifikapo mwezi Februari Mwakani. 

Profesa Mbarawa ametoa kauli hiyo alipokuwa akikagu kazi ya Ujenzi na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza pamoja na daraja la furahisha jijini Mwanza. 

Profesa Mbarawa amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi na Upanuzi wa uwanja huo kutaimarisha hali ya usafiri wa anga kwa wakazi wa Mwanza na Mikoa mingine na hivyo kukuza shughuli za kibiashara nchini. 

“Hakikisheni upanuzi wa uwanja wa ndege huu unakamilika haraka ili kurahisisha na kuboresha huduma za usafirishaji wa anga kiwanjani hapa”, amesema Waziri Mbarawa. 

Aidha, Profesa Mbarawa amewataka wakandarasi wa makampuni ya kumalizika kwa wakati upanuzi wa barabara ya kwenda Uwanja wa ndege wa Mwanza (km 9.15) pamoja na daraja la watembea kwa miguu la furahisha ambavyo kwa pamoja vitasaidia kukuza uchumi katika jiji la Mwanza. 

Amewataka wananchi wa Mwanza kutoharibu miundo mbinu ya barabara na madaraja ambapo Serikali inatumia gharama kubwa katika utengenezaji wake. 

“Naomba muitunze na kuithamini miundombinu hii kwani serikali inatumia gharama kubwa katika kutengeneza miundo mbinu hii ambayo ni muhimu kwa jamii na nchi kwa ujumla”, amesisitza Profesa Mbarawa. 

Ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza ni mkakati wa Serikali kupiti Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhakikisha kuwa katika bajeti ya mwaka 2016/2017 inatoa fedha kwa lengo la kuhakikisha ujenzi wa uwanja wa ndege huu unaboreshwa kuwa wa kisasa ili kuwezesha ndege kubwa kutua kwa wingi lakini pia kutumiwa kimataifa na nchi za Maziwa Makuu kama alivyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2015.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA