Sunday 25 September 2016

WEST HAM YAZIDI KUWA VIBONDE LIGI KUU ENGLAND, YAPIGWA 3:0 NA SOUTHAMPTON

Mchezaji Charlie Austin amefunga goli lake la tano katika michezo minne wakati Southampton ikiiadhibu West Ham kwa magoli 3-0 ikiwa ni kipigo cha nne mfululizo cha Ligi Kuu ya Uingereza.

Austin alikuwa wa kwanza kuifungia Southampton kufuatia shambuli kali na kisha Dusan Tadic akaongeza la pili akipokea pasi ya Austin na kumzungusha Adrian kabla ya kutikisa nyavu.

James Ward-Prowse alikamilisha karamu ya magoli kwa kufunga goli la tatu kwa shuti la chini na kuiacha West Ham ikiwa haijapata ushindi wowote katika dimba lao jipya la London.
                                   Mshambuliaji Charlie Austin akiachia shuti lililojaa wavuni 
     Dusan Tadic akiwania mpira ambao alifanikiwa kumzidi maarifa kipa Adrian na kuandika goli

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA