ACT YAZINDUA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA JIJINI DAR


Mmoja ya waumini akisoma neno la Mungu wakati Mchungaji akiwaongoza

Waumini wakimsikiliza kwa makini Baba Mchungaji akifundisha neno

Katibu wa kamati ya ujenzi Debora Simon (wa kwanza Kulia) pamoja na waumini mwengine wakifuatilia neno

Mchungaji wa Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele akiendelea kutoa mahubiri wakati wa Ibada hiyo ya uzinduzi wa Harambee ya uchangiaji kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa

Mweka Hazina wa Kanisa hilo Bwana Geofrey Raymond akifuatilia Ibada kwa makini

Waumini wakiendelea kufuatilia Ibada kwa makini

Mmoja wa watoto akisoma Neno la Mungu wakati wa Ibada hiyo ya Uchangiaji kwa ajili ya Ujenzi wa Kanisa

Wakijiandaa Kumtukuza Mungu

Baadhi ya watoto wakiwa Ibadani

Mchungaji wa Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele akiimba nyimbo za Sifa

Mweka Hazina wa Kanisa hilo Bwana Geofrey Raymond akizungumza neno wakati wa Ibada hiyo

Ibrahim Chanikicha Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi akizungumza jambo

Waimbaji wakiendelea kumtukuza Mungu kwa njia ya Nyimbo za Sifa

Waumini wakiimba nyimbo za Sifa

Muda wa Maombezi ulifika ambapo Mchungaji wa Kanisa
la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele aliwaombea watumishi mbali mbali
la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele aliwaombea watumishi mbali mbali

Wakiendelea kusifu na Kuabudu Picha zote na Fredy Njeje
Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) linaloendesha shughuli zake katika ukumbi wa Utoji, Sinza Mapambano jijini Dar limezindua harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo rasmi .
Akizungumza katika misa iliyofanyika eneo hilo, mchungaji wa kanisa hilo Pastor Sos Mabele alisema kuwa harambee hiyo imezinduliwa kanisani hapo kwa waumini na watu mbalimbali kuweka ahadi au kuchangia moja kwa moja fedha kwa ajili ya ujenzi wa kanisa unaotarajiwa kuanza mwisho wa mwaka huu.
Mbali na hayo Mchungaji huyo aliwataka watu mbalimbali wajitokeze kuchangia ujenzi wa kanisa hilo bila kujali madhehebu au dini, kwa kuwa Mungu ni wa wote ambapo pia alisema kuwa zoezi la harambee litaisha tarehe 25 mwezi huu kwa walioahidi wote kutimiza ahadi zao.
“Sisi kanisa letu kama linavyosema kuwa ni All- Nations Christian Tabernacle yaani hekalu la makanisa ya mataifa yote, hivyo hatubagui mtu kwa dhehebu wala dini na wote wanakaribishwa kila jumapili kwenye ibada zetu,” alisema Pastor Sos na kuwataka watu waendelee kuwasiliana naye kwa ahadi na michango kupitia namba 0784935855.
Naye mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Kanisa hilo, bwana Ibrahimu Chanikicha, aliwashukuru wote wanaoendelea kuchangia kwa hali na mali na kuwaomba waendelee kuwa na moyo huohuyo.
0 comments:
Post a Comment