Saturday, 29 October 2016

JESHI LA NIGERIA LAWAACHILIA WATOTO 876

Wanajeshi huwazuilia raia ambao wamekuwa wakiishi maeneo ya wanamgambo
Umoja wa Mataifa umefanikisha kuachiliwa kwa watoto 876 wanaozuiliwa na wanajeshi wa Nigeria na vikosi vya usalama baada ya kuteka ardhi iliyokuwa ikikaliwa na Boko Haram.
Watoto hao wamekuwa wakizuiliwa katika kambi za kijeshi kwenye mji wa Maiduguri ulio Kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Wanajeshi huwazuilia raia ambao wamekuwa wakiishi maeneo ambayo yamekuwa yakikaliwa na wanamgambo wa kiislamu, kwa kuwashukuwa kwa wana uhusiano na shughuli za wanamgambo hao.
Hata hivyo makundi ya kibinadamu yanalalamika kuwa hakuna sheria ya kuwafungulia mashtaka watu hao.
Baadhi yao hupelekwa kwa vituo vya kurekebisha tabia ambavyo makundi ya kibinadamu yanasema kuwa vinafanana na magereza.
-BBC

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA