Saturday 15 October 2016

MAELFU YA WAOMBOLEZAJI WAJIPANGA KWENYE MITAA YA BANGKOK


Maelfu ya waombolezaji nchini Thailand wamejipanga kwenye Mitaa ya Bangkok, wakati mwili wa Mfalme wao Bhumibol Adulyadej ukitolewa hospitali na kupelekwa kwenye jumba la mfalme.

Mfalme huyo aliyekaa madarakani kwa muda mrefu kuliko wote duniani alifariki dunia jana Alhamis akiwa na miaka 88 baada ya kuugua, na kulifanya taifa hilo kuingia kwenye maombolezo.

Serikali ya Thailand imetangaza maombolezo rasmi ya mwaka mzima. Mwana wa mfalme huyo Maha Vajiralongkorn ametajwa kuwa ni mrithi wake, lakini ameomba kucheleweshwa kwa mchakato wake.
                Waombolezaji wakiwa wamejipanga kungojea kuona mwili wa mfalme wao 

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA