Tuesday 4 October 2016

ESTONIA YAANDIKA HISTORIA MPYA , YAPATA RAIS WA KWANZA MWANAMKE



Bunge la Estonia limemchagua Kersti Kaljulaid kuwa rais wa nchi hiyo katika uchaguzi uliofanyika jana nchini humo.

Kaljulaid anakuwa mwanamke wa kwanza kuwa Rais nchini humo na anatarajiwa kuapa mnamo Oktoba 10.

Kabla ya uchaguzi huo, uliofanywa katika hatua tatu, Kadri Simson kwa niaba ya wabunge 31 wakiongozwa na Rais wa Bunge hilo, Eiki Nestor, walifanya mabadiliko ya katiba ili kuwepo kwa uchaguzi wa moja kwa moja badala ya kura kupigwa na wabunge.

Katika uchaguzi huo wabunge 98 kati ya 101, walijiandikisha kuwepo bungeni na upigaji wa kura ulianza saa 7:12 mchana.

Uchaguzi ulimalizika saa 8:12, boksi la kura lilifunguliwa mbele ya bunge ambapo kati ya kura 98 zilizopigwa, 81 zilimchagua Kaljulaid kuwa rais. Kati ya hizo zilizoharibika zilikuwa 17.

Eiki Nestor, Rais wa bunge, alimtangaza Kaljulaid kuwa rais wa nchi hiyo

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA