UBER YAZINDUA HUDUMA YA MADEREVA NA WASAFIRI KUCHATI KWA KUTUMIA PROGRAMU HIYO
Dar es Salaam
Tarehe 21 Agosti 2017…Kampuni ya Uber nchini Tanzania imetangaza zana mpya
maarufu kama “Kuchati Ndani ya Programu” inayowawezesha madereva na wasafiri
kuandikiana ujumbe kwa kutumia programu hiyo bila malipo.
Kinyume na hapo
awali ambapo madereva na wasafiri wangetumia Ujumbe Mfupi (SMS) au kupiga simu,
zana hii inaleta unafuu kwa madereva na wasafiri hivyo basi kuwapunguzia kadhia
ya gharama za kupiga simu sambamba na kuharakisha mawasiliano bila kuondoka kwenye
programu ya Uber.
Maboresho haya ni
juhudi endelevu za Uber na yanalenga kuimarisha wigo wa wasafiri na madereva
wanapotumia programu ya Uber.
Zana hii mpya ni
rahisi sana kuitumia. Msafiri anapoita gari, kuna kitufe cha ‘Kuwasiliana’
kwenye menyu inayoonekana chini ya skrini. Wasafiri wanaweza kuwaandikia ujumbe
madereva, na madereva vivyo hivyo. Ujumbe utaonesha kwamba umepokelewa baada ya
kuutuma.
Kwa upande
mwingine, madereva watakiri kwamba wamesoma ujumbe kwa kugusa kwenye programu
ya Uber ili watume ujumbe wa ‘bomba’. Ili wasijichanganye barabarani.
Aidha wasafiri na madereva wanaweza kuona kama ujumbe wao waliotuma umesomwa.
Meneja Msimamizi wa
Uber nchini Tanzania Bw. Alfred Msemo amehoji kwamba, “Kila safari nzuri huanza
pale msafiri anapochukuliwa kwa gari, kwa hiyo tunajituma kutafuta mbinu za
kumchukua msafiri bila usumbufu wowote kwa msafiri au dereva. Kipengele hiki
cha Kuchati kitakuwa afueni kwa wasafiri na madereva wanapotaka kuwasiliana ili
kusaidiana kutafuta mwafaka wa changamoto za safari kama vile, kufungwa kwa
barabara au kutoa maelezo ya mahali walipo.”
Kadhalika,
kipengele hiki kinatoa njia mbadala ya wasafiri na madereva kupiga simu
wanapotaka kuwasiliana. Hata hivyo, ili mtu atumie kipengele hiki anatakiwa awe
anatumia toleo la sasa la program ya Uber.
“Huu ni mwanzo tu
wa mchakato wa kuimarisha huduma za kutuma ujumbe moja kwa moja kwenye programu
ili kufanikisha wigo wa mawasiliano yasiyo na changamoto kwa wateja wetu, na
kuwasaidia kuwasiliana katika ulimwengu wa utandawazi na ulimwengu halisi”
amenukuliwa Bw. Msemo.
0 comments:
Post a Comment