Tuesday, 1 November 2016

FUNGUKA LIVE:: WIZARA YA ELIMU,WAPI TUNAELEKEA??

Image result for a puzzled cartoon
Jaman wizara ya elimu, wapi tunaelekea?
Mbona mambo hayaeleweki taratibu zinabadilika kila kukicha, nini tatizo? 
Maamuzi yanafanyika pasipo tathimini ya kutosha kwa maslahi ya watanzania wote?
Mama Ndalichako ni nini unafanya?

Umma wa wawatanzania unakosa kupata haki zao stahiki za kielimu, elimu ni jambo muhimu kwa mwanadamu linaloweza kumletea mwanadamu ukombozi wa kifukra na akaweza kujitegemea katika nyanja mbalimbali endapo atapewa elimu bora.

Mambo yamekuwa yakibadilika siku hadi siku, taratibu za udahili wa wanafunzi vyuoni, utoaji wa mikopo, madaraja ya ufaulu n.k

Wizara ya elimu; ni miongoni mwa wizara muhimu sana katika maendeleo ya Taifa lolote, 
Mwl. Nyerere alisema ili kuyafikia maendeleo ni lazima tupige vita.
+Ujinga
+Umaskini
+Maradhi.

Ujinga unatibiwa na daktari wa ujinga ambaye ni mwalimu.

Je, maslahi ya walimu yanaboreshwa?

Wizara ya elimu kila siku inalalamika kunauhaba mkubwa wa walimu wa sayansi wakati walimu wasayansi waliofuzu wapo mtaani hawana kazi.

Binadamu tunaishi kwa kutegemeana, hivyo kila mtu ana impact kwa mwenzake, miongoni mwa vipaumbele vya serikali ni masomo ya sayansi ni jambo jema lakini hatuwezi kuwa na taifa la wanasayansi tuuuuuu ni lazma wawepo wataalamu wa nyanja mbalimbali kama vile, wanasheria, maafisa maendeleo, washauri, maafisa ugavi maafisa manunuzi, maafisa mahusiano wahasibu maafisa masoko, walimu wa sayansi, biashara na sana n.k

Ajira za elimu, ndizo zinazo zalisha wataalamu mbalimbali katika nyanja tofauti.

Mhasibu ni lazima awe amemasomo ya biashara, Mwanasheria ni lazima awe amesoma masomo ya sanaa
Mhandisi pia ni lazima awe amesoma masomo ya sayansi.
Sasa watu hawa wote katika taasisi yoyote wanategemeana na kila mmoja ana umuhimu wake.

Swala la serikali kusema haita toa ajira kwa walimu wasio wa masomo ya sayansi binafsi naona kuna makosa, na pia Mh. Waziri wa Elimu aliposema serikali ina mpango wa kuweka ulazima wa masomo ya sayansi kwa wanafunzi wa sekondari binafsi naona si sawa kwani mazingira hayajaandaliwa kufanya jambo hilo, lakini pia wanafunzi wanahulka ama interest tofauti huwezi kusema eti ni lazima wasome sayansi huko ni kudharau fani zisizo za sayansi pamoja na mchango mkubwa kwa Taifa letu. 

Walimu wa sanaa c kwamba ni wengi sana kiasi kwamba wametosheleza na serikali haiwezi kuwaajiri, walimu wapo wengi mijini pekee vijijini kuna uhaba wa waalimu kwa kiwango kikubwa; shida IPO katika allocation of human resources(Teachers) jambo hilo ndo linafanya shule za mijini kuwa na idadi kubwa ya walimu ukilinganisha na shule za vijijini: Serikali ingeandaa mpango maalumu wa kuallocate walimu direct kulingana na uhitaji asilia wa shule husika kutoka maeneo mbalimbali ya nchi yetu.

Kuna changamoto nyingi sana hususani katika sekta ya elimu lakini hazina budi kupewa kipaumbele kwani ni sekta muhimu kwa maendeleo ya Taifa letu.

Tafiti nyingi sana zinafanywa na wafunzi wa vyuo vikuu kila mwaka, wataalamu wa elimu na wadau mbalimbali wa elimu katika taifa letu laiti kama zingekuwa zinafanyiwa kazi sekta ya elimu ingeweza kupiga hatua kubwa sana, tafiti nyingi zinafanywa lakini hazifanyiwi kazi hili ni tatizo kubwa sana.

Mikopo.

Wanafunzi wa vyuo vikuu ni haki yao kupata mkopo kwani si fedha ya bure ni fedha ambayo mwanafunzi anakopeshwa kwa ajili ya kupata elimu na baadae anapaswa kuirudisha, endapo ana sifa stahiki za kupata mkopo huo.

Bodi ya mikopo inachotaka kufanya si sahihi kulingana na mtazamo wangu;

Huwezi badilisha taratibu za upataji wa mikopo kwa mwanafunzi aliyepata mkopo anayeendelea na masomo yake kwani hapo awali alikidhi vigezo na akastahiki kupata mkopo iwaje leo ubadilishe vigezo na kutumia vigezo vipya kubaini ustahiki wake wa kupata mkopo, kama ni utaratibu mpya au vigezo vipya basi vianze na wanafunzi wapya wanaodahiliwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Pia serikali ingefanya tathmini ya kutosha katika swala zima la utoaji wa mikopo kwa wanafunzi, maisha ya chuo ni magumu sana kiuchumi serikali ingejitahidi walau kila mwanafunzi apate walau hata fedha ya accomidation ila wasio na uwezo kabisa ndo walipiwe ada.

#Wizara ya Elimu haihitaji siasa inahitaji mipango madhubuti na endelevu ya kitaalamu kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa letu.
Kumekua na myumbisho mkubwa katika sekta hii Tangu kipindi cha Mungai mpaka sasa kwa Mh. Ndalichako jambo ambalo linaathiri ubora wa elimu yetu kwani kila kiongozi anaingia madarakani na mipango yake.

Chanagmoto ni nyingi sana katika sekta ya Elimu kwa leo naomba niishie hapa✍🏼


Email. msyangi93@gmail.com
 MSYANGI M. KURUCHUMILA.
0655-950-324

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA