MESSI MWANASOKA BORA WA DUNIA KWA MARA YA TANO,AWAPIKU RONALDO , NEYMAR
Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi akiwa na tuzo yake ya Ballon d'Or baada ya kukaabidhiwa usiku huu.
NYOTA wa Barcelona, Muargentina Lionel Messi ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia kwa mara ya tano.
Messi
amenyakua Ballon d’Or ya FIFA akiwabwaga wapinzani wake, Mbrazil Neymar
anayecheza naye Barca na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid katika hafla
inayoendelea usiku huu mjini Zurich, Uswisi.
Lionel Messi amepata asilimia 41.33 ya kura zote akifuatiwa na Cristiano Ronaldo wa Ureno aliyepata asilimia 27.76, wakati Neymar anayeingia fainali kwa mara ya kwanza, amepata asilimia 7.86.
Mafanikio
hayo yanakuja baada ya Messi kucheza mechi 53 mwaka jana akiwa na
Barcelona, kufunga mabao 48 na kusababisha mabao 23, ingawa Cristiano
Ronaldo alifanya vizuri zaidi, akifunga mabao 54 katika mechi 52 za Real
Madrid.
Kikosi
Bora cha Dunia cha Mwaka 2015; Kutoka kushoto; Thiago Silva, Luka
Modric Marcelo, Paul Pogba, Sergio Ramos, Neymar, Dani Alves, Lionel
Messi, Andres Iniesta na Cristiano Ronaldo katika picha ya pamoja baada
ya kutangazwa usiku huu Zurich.
picha na Dailymail.
picha na Dailymail.
0 comments:
Post a Comment