TAARIFA KUHUSU TAHARUKI YA MOTO ULIOLIPUKA KWENYE BANDARI YA DAR ES SALAAM
Jana Nov 1 2016 katika Bandari ya Dar es salaam kulitokea moto ambao ulizua taharuki kwa baadhi ya wafanyakazi na watu wengine waliokuwa eneo hilo la bandari.
Moto huo ulilipuka kwenye makontena na kuteketeza kontena tatu zilizokuwa na matairi ya magari na kudumu kwa muda wa dakika 30.
Mkuu wa mawasiliano wa mamlaka ya Bandari, Peter Mlanzi ametoa ufafanuzi kuhusu moto huo kwamba uliandaliwa makusudi kwa ajili ya kukipima kikosi cha zima moto…
"Tukio hili tumelitengeza kwa makusudi ili tuone namna ambavyo kikosi kazi cha zimamoto na uokoaji kinavyoweza kukabilana na majanga mbalimbali" Alisema Mlanzi
Aidha kwa upande wake mkuu wa kikosi cha zimamoto bandari ya Dar es salaam, Mussa Biboze, alisema' "kwa zimamoto moto uko kwenye madaraja, huu moto wa matairi ni moto wa daraja A ambao unazimwa tu na maji ya kawaida"
0 comments:
Post a Comment