WANAFUNZI WA VYUO VIKUU KENYA WANASWA WAKIWAFANYIA MITIHANI WANAFUNZI WA SEKONDARI
Wanafunzi wawili wa Chuo Kikuu wamekamatwa katika kituo cha kufanyia mitihani kwa wanafunzi binafsi cha Makadara, Jijini Nairobi baada ya kukutwa wakiwafanyia Mitihani wa Taifa wa Sekondari wengine.
Mmoja wa watuhumiwa Alice Ahunyes, alikuwa anamfanyia mtihani Scholastica Wanjiru mwenye nambari ya mtihani 2090101144 ambaye ni mfanyabiashara aliyeenda Ghana kununua bidhaa za duka lake.
Mtuhumiwa mwingine, Salome Ondusa ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kenyatta, alilipwa shilingi 10,000 na mwanafunzi binafsi Anne Erastus mwenye namba ya mtihani 2090101177 ili amfanyie mtihani.
0 comments:
Post a Comment