Tuesday 10 January 2017

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MJUMBE MAALUM WA RAIS BUHARI WA NIGERIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 10 Januari, 2017 amekutana na kufanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Rais wa Nigeria Profesa Ibrahim Gambari nyumbani kwake Chato Mkoani Geita. Mazungumzo yao yalilenga masuala mbalimbali ya uhusiano kati ya Tanzania na Nigeria.

Rais Magufuli amempongeza Rais Muhammadu Buhari kwa jitihada kubwa anazochukua kwa ajili ya kuleta maendeleo nchini mwaka.

Pia, Rais Magufuli amempongeza Rais Buhari kwa jitihada anazozifanya za kukabiliana na kundi la Boko haramu ili kuhakikisha amani inaendelea kudumu nchini mwake.

Kwa upande wake Mjumbe Maalum wa Rais wa Nigeria, Profesa Ibrahim Gambari amempongeza Rais Magufuli kwa ushindi alioupata na jitihada anazochukua katika kupambana na rushwa na kubana matumizi jambo ambalo linaungwa mkono na wananchi wengi wa Nigeria.

Profesa Gambari alimkabidhi Rais Magufuli barua yenye ujumbe maalum kutoka kwa Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Chato, Geita
10 Januari, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na Profesa Ibrahim Gambari ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais wa Nigeria Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea barua yenye ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari uliowasilishwa na Profesa Ibrahim Gambari ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais huyo wa Nigeria, Chato mkoani Geita.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA