Showing posts with label rais magufuli. Show all posts
Showing posts with label rais magufuli. Show all posts

Monday, 30 October 2017

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AHUTUBIA WAKAZI WA NYAKATO MKOANI MWANZA

1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Nyakato nje kidogo ya jiji la Mwanza mara baada ya kufungua kiwandaa cha Sayona Drinks ltd kilichopo Nyakato.

3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Katikati ya jiji la  Mwanza wakati akitokea Nyakato.
7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi wakati mmiliki wa Kiwanda cha Sayona Drinks Subhas Patel alipokuwa akionesha bidhaa mojawapo ya kiwanda hicho.
9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na Mke wake Mama Janeth Magufuli pamoja  mbunge wa Ilemela Angelina Mabula wakati Kwaya ya Makongoro ilipokuwa ikitumbuza katika viwanja vya Mwatex Nyakato jijini Mwanza
10
Kwaya ya Makongoro ikitumbuiza
11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza kwa makini wimbo wa kwaya ya Makongoro kabla ya kuhutubia mamia ya wananchi Nyakato mkoani Mwanza.
13
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na wananchi wa Nyakato mara baada ya kuwahutubia.
16
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kuagana na Wananchi wa Nyakato  mara baada ya kumaliza kuwahutubia. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kuagana na Wananchi wa Nyakato  mara baada ya kumaliza kuwahutubia.
17
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kiwanda cha Sayona Drinks kilichopo Nyakato jijini Mwanza.
PICHA NA IKULU

Monday, 21 August 2017

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA RAIS WA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA MAENDELEO LA JAPAN (JICA)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  tarehe 21 Agosti, 2017 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA),Bwana Shinichi Kitaoka Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Katika Mazungumzo hayo Bw. Kitaoka amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa uongozi mzuri na wa mfano hususani katika kupambana na rushwa na msukumo mkubwa anaoutoa katika maendeleo hususani katika kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Jitihada  zinazosaidia kuimarisha uchumi na kuboresha huduma za kijamii na kuahidi kuwa JICA itaendelea kuwa mshirika mkubwa wa maendeleo kwa Tanzania.

Bw. Kitaoka ambaye ni mara yake ya kwanza kuitembelea Tanzania kama Rais wa JICA amemuahidi Rais Dkt Magufuli kuwa miradi yote ya maendeleo ya nyuma na ya sasa inayotekelezwa kwa pamoja kati ya  Tanzania na JICA itamalizika kwa wakati ikiwemo mradi wa ujenzi wa barabara za juu (Flyover) wa TAZARA unaoendelea kujengwa hivi sasa,mradi wa ujenzi wa barabara ya Mwenge - Moroco yenye urefu wa kilomita 4 nukta 3 pamoja na mradi wa ujenzi wa daraja la Gerezani.

 “Tumefikia makubaliano mazuri kuhusiana na miradi tunayoendelea kuitekeleza hapa nchini na wananchi watarajie kuona kazi zikifanyika kuanzia mwezi june,mwakani hususani katika ujenzi wa daraja la gerezani na mingineyo”

Kwa upande wake Mhe. Dkt Rais Magufuli amemshukuru Rais huyo wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan Bw. Shinichi Kitaoka kwa uamuzi wake wa kuja Tanzania na amemhakikishia kuwa Tanzania inatambua mchango mkubwa ambao Japan inautoa katika maendeleo ya Tanzania kupitia JICA, na kwamba itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake na Japan katika masuala mbalimbali.

Mhe. Rais Magufuli ameishukuru JICA kwa kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi jijini Dar es Salaam ikiwemo upanuzi wa barabara ya Mwenge – Morocco, utakaoiwezesha barabara hiyo kuwa na zaidi ya njia nane, ujenzi wa barabara ya TAZARA, ujenzi wa Daraja la Gerezani njia nne, na barabara ya Bendera tatu hadi Kamata.

 “Tunathamini sana mchango unaotolewa na walipa kodi wa Japan kupitia JICA katika kutekeleza miradi ya maendeleo hapa nchini na ninakuomba kuangalia uwezekano wa kufadhili na kujenga miundo mbinu na miradi mbalimbali ya maendeleo katika Makao Makuu ya nchi Dodoma ambako serikali imedhamiria kuhamia huko ili kuweka alama ya urafiki na mahusiano mema yaliyopo kati ya Tanzania na Japan”

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Balozi wa Japan hapa nchini Mhe. Masaharu Yoshida,Katibu Mkuu wizara ya Fedha na Mipango Doto James, Katibu Mkuu Ujenzi Mhandisi Joseph Nyamhanga na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini Mhandisi Patrick Mfugale.

Emmanuel Buhohela,
Mwandishi wa Habari,Msaidizi wa Rais,
Dar es Salaam.

21 Agosti, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo  na Rais wa shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Bw. Shinichi Kitaoka (kushoto) na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida leo agosti 21, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Joseph Nyamhanga na Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale kwa Rais wa shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Bw. Shinichi Kitaoka aliyekutana naye leo agosti 21, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam

Tuesday, 15 August 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AAGANA NA MGENI WAKE RAIS WA MISRI PIA AKUTANA NA WAZIRI WA ZAMANI WA MAMBO YA NJE WA JAPAN


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi wakati wa nyimbo za mataifa mawili zikipigwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA). Rais huyo wa Misri ameondoka mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi wakati akielekea kupanda ndege mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akicheza nyimbo za kikundi cha matarumbeta kilichokuwa kikitumbuiza katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya kumsindikiza mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi ambaye ameondoka mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge na Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Japan Ichiro Aisawa aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mbunge na Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Japan Ichiro Aisawa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mbunge na Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Japan Ichiro Aisawa mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.

                                                                                    PICHA NA IKULU

Thursday, 10 August 2017

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AKUTANA NA RAIS WA MASHIRIKA YA KIPAPA –VATICAN BABA ASKOFU PROTAS RUGAMBWA, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

1

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Rais wa Mashirika ya Kipapa-Vatican, Mhashamu Baba Askofu Protas Rugambwa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
2.-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya Sanamu ya Bikira Maria wa Fatima kutoka kwa Rais wa Mashirika ya Kipapa-Vatican, Mhashamu Baba Askofu Protas Rugambwa aliyefika Ikulu jijini Dar es Salaam
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Rozali aliyopewa na Rais wa Mashirika ya Kipapa-Vatican, Mhashamu Baba Askofu Protas Rugambwa aliyefika Ikulu jijini Dar es Salaam
5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Rais wa Mashirika ya Kipapa-Vatican, Mhashamu Baba Askofu Protas Rugambwa wapili kutoka kushoto Ikulu jijini Dar es Salaam.
6 7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza na kumuaga mgeni wake Rais wa Mashirika ya Kipapa-Vatican, Mhashamu Baba Askofu Protas Rugambwa Ikulu jijini Dar es Salaam. 

   PICHA NA IKULU

Monday, 3 July 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UBORESHAJI WA BANDARI YA DAR ES SALAAM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam katika eneo la Bandari hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
 Baadhi ya mabalozi kutoka nchi mbalimbali wakifatilia Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird mara baada ya kutoa hotuba yake kabla ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi wakati Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird alipokuwa akisoma hotuba yake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird wakati wakitazama kipeperushi ya maelezo ya Mradi wa uboreshaji wa Bandari jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird pamoja na viongozi wengine wakiimba wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili katika eneo la Bandari jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akicheza muziki pamoja na Banana Zorro, Mrisho Mpoto, pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akicheza muziki pamoja na Banana Zorro, Mrisho Mpoto, pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akicheza muziki pamoja na Banana Zorro, Mrisho Mpoto, pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma mara baada ya tukio la uwekaji wa jiwe la msingi Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na viongozi wengine waliosimama wakati Banana Zorro pamoja na Mrisho Mpoto walipokuwa wakiimbawimbo wa Aamka Tufanye kazi kabla ya tukio la uwekaji wa jiwe la msingi Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Tuesday, 6 June 2017

RAIS MAGUFULI AMUAPISHA BI.ANNA MGHWIRA KUWA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Juni, 2017 amemuapisha Bi. Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Bi. Anna Elisha Mghwira amejaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Saidi Meck Sadiki aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo.

Hafla ya kuapishwa kwa Bibi Anna Elisha Mghwira imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

Akizungumza baada ya kumuapisha, Mhe. Rais Magufuli amemtaka Bi. Anna Elisha Mghwira kwenda kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kuondoa kero zinazowakabili wananchi wa Kilimanjaro bila kujali itikadi za vyama vyao vya siasa, dini, makabilia na kanda wanazotoka.

Mhe. Rais Magufuli amemhakikishia kuwa atapata ushirikiano wa kutosha wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake na asikubali kuyumbishwa na mtu yeyote katika majukumu yake ya kuwahudumia wananchi.

“Mimi huwa siteui watu hivi hivi, huwa naangalia uwezo wa mtu, na wewe nimekuchunguza na nimejiridhisha kuwa una uwezo wa kuwatumikia wananchi, nenda kachape kazi, kawaondolee kero wananchi wa Kilimanjaro, wapo watu watakaokusema na wengine watakuonea wivu, wewe kachape kazi” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Kwa upande wake Bi.Anna Elisha Mghwira amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na amemuahidi kuwa yupo tayari kwenda kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi na kujenga Taifa.

“Ninasema hii ni heshima kwa Taifa letu, ni heshima kwa umoja wa nchi yetu, ni heshima kwa siasa za umoja wa nchi yetu, kumekuwa na minong’ono mingi sana kuwa Rais analeta nini, kuteua watu wanaitwa wapinzani, mimi sio mpinzani wa maendeleo” amesema Bi. Mghwira. 


Friday, 2 June 2017

RAIS MAGUFULI ATOA MAAGIZO MAZITO KWA IGP SIMON SIRRO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi nchini kutumia weledi wake kwa kiwango cha juu katika kutekeleza jukumu lake lakulinda raia na mali zao, hasa kukomesha vitendo vya uhalifu.

Mhe. Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 02 Juni, 2017wakati akizungumza na Makamanda Wakuu kutoka makao makuu ya polisi, Makamanda wa Mikoa na Vikosi vya Tanzania Bara na Zanzibar na viongozi wote wakuu wa polisi wa Mkoa wa Dar es Salaam waliokutanakatika Bwalo la Maofisa Wakuu wa polisi lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Dkt. Magufuli amelipongeza Jeshi la Polisi kwa juhudi zake za kukabiliana na uhalifu lakini ametaka juhudi hizo ziongezwe hususanikukabiliana na matukio ya ujambazi na mauaji ya raia, dawa za kulevya na kuendesha operesheni zenye tija katika mikoa yote.

Amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro kujipanga vizuri yeye na safu yake ya Makamanda, Viongozi Wakuu wa Vikosi na Maofisa mbalimbali ili kuondoa dosari zote za utendaji kazi zinazoshusha ufanisi na heshima ya Jeshi la Polisi.

“Ni lazima ufanye mabadiliko makubwa, nataka kuona Jeshi la Polisi linakuwa Jeshi la Polisi, Wewe IGP Sirro na Makamnda wenzako hakikisheni mnakomesha uhalifu, komesheni mauaji dhidi ya raia, ujambazi na dawa za kulevya” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewataka Makamanda, Maofisana Askari wa jeshi hilo kujiepusha na rushwa, dawa za kulevya, kutumiwa na watu kwa maslai binafsi, kuingia mikataba isiyo na maslai kwa Jeshi na Taifa, ubadhirifu na kuacha upendeleo katika utoaji wa ajira na vyeo.

Mhe. Rais Magufuli pia ametaka Makamanda, Maofisa na Askari wote wa Jeshi la Polisi wampe ushirikiano wa kutosha IGP Simon Sirro ambaye hivi karibuni amemteua kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Mstaafu Projest Rwegasira.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
02 Juni, 2017
 

Monday, 15 May 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AIFUTA MAMLAKA YA USTAWISHAJI MAKAO MAKUU CDA, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Displaying 1.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Amri ya Rais (Presidential Order) kuifuta   Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Displaying 5.jpg

Displaying 7.jpg



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasilikiza viongozi mbalimbali waliokuwa wakichangia mara baada ya kusaini Amri ya Rais (Presidential Order) kuifuta   Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA,tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam


Displaying 10.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kusaini Amri ya Rais (Presidential Order) kuifuta   Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.


Displaying 12.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Ardhi William Lukuvi, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi kuhusu uamuzi wake wa kuifuta   Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA,tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU

Thursday, 11 May 2017

RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA MGENI WAKE RAIS WA AFRIKA KUSINI JACOB ZUMA WAHUDHURIA KATIKA JUKWAA LA WAFANYABIASHARA JIJINI DAR ES SALAAM

unnamed
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wafanyabiashara mbalimbali wa nchini pamoja na Afrika ya Kusini wakati aliposhiriki pamoja na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma katika Jukwaa hilo la Wafanyabiashara jijini Dar es Salaam.

A 1
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akisoma hotuba yake katika Jukwaa hilo la Wafanyabiashara wa Tanzania na Afrika Kusini lililofanyika jijini Dar es Salaam.
A 2
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kutoka kwenye Jukwaa hilo la Wafanyabiashara wa Tanzania na Afrika Kusini lililofanyika jijini Dar es Salaam.
A 3
Sehemu ya Wafanyabiashara mbalimbali wa Tanzania na Afrika Kusini waliohudhuria katika Jukwaa hilo la Wafanyabiashara jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA