TCAA YAZINDUA RASMI MAFUNZO YA URUSHAJI NDEGE ZISIZO NA RUBANI "DRONES"
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S.Johari akifungua rasmi awamu ya kwanza ya mafunzo ya ndege zisizo na rubani maarufu kama ndege nyuki(drone),mafunzo hayo yanatolewa na Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC)kinachomilikiwa na TCAA kwa ushirikiano na chuo cha Pro Wings kutoka Afrika ya Kusini, yanafanyika kwa muda wa wiki nne(moja darasani , tatu mafunzo kwa vitendo.)
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC)kinachomilikiwa na TCAA, Aristid Kanje akielezea muhtasari wa mafunzo hayo wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo ya wiki nne kuanzia Januari nne 2021.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Pro Wings kutoka nchini Afrika ya Kusini,Benjamin Mabeta akiwakaribisha washiriki na kueleza yale watakayojifunza katika muda huo wa wiki nne.
Washiriki wa mafunzo ya awamu ya kwanza ya mafunzo ya ndege zisizo na rubani maarufu kama ndege nyuki(drone) wakifuatilia ufunguzi rasmi ya mafunzo hayo.mafunzo hayo yanatolewa na Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC)kinachomilikiwa na TCAA kwa ushirikiano na chuo cha Pro Wings kutoka Afrika ya Kusini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S.Johari(aliyeshika ndege nyuki) akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu na washiriki , baada ya kufungua rasmi awamu ya kwanza ya mafunzo ya ndege zisizo na rubani maarufu kama ndege nyuki(drone),mafunzo hayo yanatolewa na Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC)kinachomilikiwa na TCAA kwa ushirikiano na chuo cha Pro Wings kutoka Afrika ya Kusini, yanafanyika kwa muda wa wiki nne(moja darasani , tatu mafunzo kwa vitendo.)
0 comments:
Post a Comment