JE UNAWEZA KUPANGILIA RANGI KWENYE MAVAZI YAKO?!
Na Jackline Ngapemba
Hakuna mtu anayejua kila kitu. Ni wazi hata sisi hatujui kila kitu. Pamoja na hayo, tunapenda sana kujifunza.Tunajifunza kwa niaba yetu na kwa niaba yako msomaji. Yale tunayojifunza tunajaribu kukushirikisha ili tusaidiane
Ukipangilia nguo zako kwa kufatilia rangi zinazoshabihiana kama zinavyoonekana kwenye duara la rangi ndivyo utakavyopendeza zaidi, rangi zinazoshabihiana huletakujiamini na kukufanya uonekane kama mvaaji anaejua nguo na kufahamu rangi na kuzivaa kuendana na mpangilio wa jinsi unavyotakiwa na muonekano makini zaidi.
1. Rangi nyeupe inaendana na kila rangi ya nguo. Pale kila kitu kinaposhindikana nyanyua rangi nyeupe, rangi nyeupe huendana na kila rangi ya kila nguo uliyonayo. Hasa rangi ya zile nguo ambazo huwa unashindwa jinsi ya kuzipangilia na nguo nyingine, unaweza kuivaa na tai ya rangi ya mistari mistari kama unataka kuvaa tai, au unaweza kuvaa pamoja na sweta lenye kola ya V. Kwa vyovyote vile utatoka bomba na kutokelezea kwa utanashati zaidi.
2. Vaa nguo zenye mng'ao wa kuendana pamoja. Ili uweze kutokelezea vizuri zaidi kwa mvuto zaidi, hakikisha thamani ya rangi ziwe zinaendana, nikiongelea thamani ya rangi namaanisha mng'ao wa nguo uwe unaendana, kama umevaa suruali rangi butu ambayo haing'ai basi na shati lazima vile vile iwe rangi butu ambayo haing'ai, na kama vile vile umevaa rangi ya kung'aa, hakikisha pia rangi fuatilizi iwe na mng'ao, Hii haimaanishi ndio uvae rangi zote ziwe na mng'ao wa kupitiliza, hapa tunazungumzia uzito wa rangi.
3. Usivae nguo yoyote ya chini yenye mng'ao wa kupitiliza. Hata kama uwe nani hakikisha unapinga hamu yeyote ya kuvaa nguo ya chini ambayo inatengeneza mng'ao, iwe ni suruali ya kitambaa, Sketi, jinzi au nguo yeyote.
Hakikisha chochote unachokivaa chini kisiwe na rangi angavu ya kushitua kuliko shati, blauzi au tisheti uliyoivaa, suruali ndio msingi wa uvaaji nguo, nguo ya chini yoyoote inatakiwa isiwe na rangi kushinda rangi ya nguo ya juu uliyoivaa.
0 comments:
Post a Comment