Tuesday, 30 November 2021

JIFUNZE HAPA NAMNA YA KUBORESHA MUONEKANO WAKO


Na Jackline Ngapemba

Kwa wavulana kuonekana upo fashionable ni rahisi mno kwa sababu fashion zao hazibadiliki mara kwa mara kama una viatu vizuri, suruali au kaptura nzuri na shirt au t-shirt nzuri basi ukivaa utaonekana umependeza lakini ni vipi uonekane stylish? ukiachana tu na kuvaa ulivyo vizoea?

Badilisha Muonekano: Tumezoea kuvaa t-shirt/shirt au suruali tukiwa tumeziachia lakini unaweza kuboresha muonekano wako kuonekana wa tofauti kwa kukunja mikono ya shirt au t-shirt lakini pia una weza kukunja miguu ya suruali.

Add layers kwenye mavazi yako: Kuongezea layers ni kuongeza nguo juu ya nguo yaani kama kuvaa coat la suit juu ya t-shirt, kuvaa kimono na kadharika.

Accessories: kama ambavyo ilivyo kwa wadada kuvaa hereni,vikuku au mikufu ndivyo hivyo hivyo kwa wakaka pia ina apply accessories zinaweka ku upgrade muonekano wako kutoka 0-100%, inaweza kuwa saa, mkanda, bracelets etc.

Uchaguzi wa rangi: Kwa ushauri wangu nguo nzuri kununua ni neutral color kama nude, grey, nyeupe, nyeusi nakadhalika ina kuwa rahisi kuvaa na rangi nyingine kama floral shirts, printed t-shirt au hata neutral on neutral ina pendeza hivyo kabati lako liwe na rangi za design hii nyingi kuliko rangi za kuwaka au zenye maua maua ili uwe na uwezo wa kubadilisha na ku style mara nyingi uwezavyo.

Wekeza katika mavazi unayo weza kuvaa mara mbili mbili – usinunue kitu kwa sababu tu kipo kwenye trend, vipi kama trend ikiisha una weza kukivaa tena? nunua nguo ambazo zinaweza kuvalika hata kama haipo kwenye trend wakati huo kuna zile trend zisizo isha kama jeans,t-shirts,flats shoes, raba nakadhalika hii itakusaidia kuto kuwa na uhitaji wa kununua nguo au viatu mara nyingi nyingi.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA