HUYU NDIYE MNYAMA ALAMA YA GUNDU VISIWA VYA MADAGASCAR
Unaweza kudhani wanyama wanaotumika kama kitoweo ndio hawana bahati njema sana,HAPANA ukipata nafasi ya kusema na Aye-Aye utagundua kuwa hali yake ni mbaya zaidi.
Aye-Aye ni nani?
Ni mnyama mwenye umbo la udogo wa kati anayepatikana katika visiwa vya Madagascar, macho makubwa yanayowaka, vidole virefu vyenye kucha ngumu, mkia mrefu na mkubwa uliofichwa na manyoa mengi yalitotapakaa mwili mzima.
Visiwani humo kwa baadhi ya kabila mnyama huyu ni maarufu sana kama alama ya nuksi iletayo mabalaa hivyo huuwawa mara moja pale anapoonekana.Dhana hii ilipelekea kupungua sana na hata kugundulika tishio la kutoweka kabisa kwa jamii ya Aye- Aye kiasi cha mamlaka husika za wanyama kulazimika kutumia sheria kuwalinda. Histoia inaonesha kuwa awali uwepo wa mnyama Aye-Aye uligundulika miaka ya 1930 na kutambulika rasmi mwaka 1957.
TISHIO HASA LA AYE-AYE LIKO WAPI?
Miongoni mwa suala kubwa linalopelekea kiumbe huyu kuwa alama ya “gundu” ni kuwa wanakijiji wanaamini kuwa kuonekana kwake maeneo ya makazi ni ishara ya kifo cha mtu, lakini wanaongeza kuwa endapo utakutana na Aye-Aye na akanyoosha kidole kukuelekea basi UTAKUFA hivyo njia pekee ya kuepusha hilo ni kumuua mara moja na kumtundika kichwa chini kwa kumning’iniza kutumia mkia wake.Kufikia mwaka 2014 mnyama Aye-Aye alitambulika kama mnyama aliyekatika hatari ya kutoweka kabisa katika uso wa dunia, Katika lugha nyepesi unaweza kusema WANAPATA TABU SANA. Sifa Kuu Ya Kitabia ya Aye- Aye ni USIRI kwani hadi sasa mnyama huyu hajawahi kushuhudiwa akijamiiana licha ya kuzaa.
Watafiti wanasema Aye- Aye anaweza kuwa mnyama pekee anayetafuta mawindo kwa kutumia mwangwi wa sauti kufahamu lilipo windo lake kitaalamu njia hii inafahamika kama ECHOLOCATION.
Na Dickson Mulashani kwa msaada wa mtandao
0 comments:
Post a Comment