Friday 5 July 2024

HATUA ZA KUKABILIANA NA UPWEKE & HUZUNI KUPITA KIASI BAADA YA MAHUSIANO KUVUNJIKA



Mahusiano kuvunjika ni jambo la kawaida kwa karne hii ya 21 kwa sababu haijalishi utakuwa na moyo wa upendo,huruma,kujali na unyenyekevu bado tabia na maamuzi ya mwenza wako yapo nje ya uwezo wako na endapo mwenza wako ameamua kuvunja mahusiano hakuna njia au mbinu ambayo unaweza kutumia kuzuia hilo.

Mahusiano yako na mwenza wako huwa yenye kugusa hisia kali sana za upendo,huruma,

Unapokuwa unampenda sana mwenza wako utawekeza pesa nyingi,muda,hisia, matumaini na mipango ya maisha yako ya baadaye.

Na endapo mahusiano yatavunjika ile hali ya upendo,huruma,kujali, unyenyekevu hugeuka kuwa chuki, wivu kupita kiasi, uchungu moyoni,hasira kupita kiasi,hisia za kisasi,upweke, kujichukia, kutamani kumdhuru mwenza wako na kumuombea mabaya.

Kitendo cha kutarajia mwenza wako kurejesha mahusiano kama zamani huku mwenza wako hayupo tayari kuendelea na mahusiano husababisha maumivu makali sana moyoni,upweke kupita kiasi,huzuni,hasira, kuchanganyikiwa, tumbo kuvurugika,moyo kwenda mbio na kizunguzungu.

Badala ya kuanza kumlaumu mwenza wako kwa màumivu ambayo unapitia baada ya  mahusiano kuvunjika unatakiwa kukubaliana na hali halisi kwamba mahusiano yamevunjika tayari na huyo hakuwa mtu sahihi katika maisha yako.

Hakuna mtu anayeweza kuziumiza hisia zako kama yule ambaye kuna kitu unatarajia kutoka kwake ili uwe na furaha.

Kama kuna kitu unakitaka kwa nguvu zote  kutoka kwa mtu yeyote lazima utakuwa na hasira,huzuni, maumivu makali sana moyoni juu ya tabia ya mtu huyo.





VIFUATAVYO NI VIASHIRIA VYA MAHUSIANO KUVUNJIKA

Mahusiano kuvunjika huwa kuna viashiria vyake ambavyo watu wengi huwa wanapuuza sana mpaka baadaye ndio huanza kulia.


1.MAWASILIANO KUPUNGUA

Kiashiria cha kwanza kwamba mahusiano yanakwenda kuvunjika ni mawasiliano kukosekana kabisa au kupungua .

Utagundua hili kwa kuona ni wewe pekee ambaye unapiga simu mfululizo, kutuma sms mfululizo ukiacha kuanzisha mawasiliano mwenzako hakutafuti na ukiuliza chochote kuhusu ukimya wake hajibu sms wala simu hapokei.

Kukosekana mawasiliano husababisha ugomvi wa mara kwa mara,kupeana vitisho,kupeana tuhuma za usaliti,kutishia kuvunja mahusiano lakini huwezi kufanya hivyo.

Mawasiliano yanapungua na hata ukifanya mawasiliano naye unabaki na hasira baada ya mazungumzo badala ya furaha.


2.UGOMVI WA MARA KWA MARA

Ugomvi wa mara kwa mara huwa kiashiria cha mahusiano kuvunjika hapa utaona kwamba kama mwenza wako akiwa mbali unakuwa na furaha na akiwa karibu yako unapata hasira sana, unatamani kupigana naye,unapata msukumo wa kumfokea, kumtukana,kumuombea mabaya.


Ugomvi unaweza kusababishwa na matukio ya usaliti wa mara kwa mara, kupoteza hisia za mapenzi juu yake, anaweza kuwa na tabia zenye maudhi ambazo mara kwa mara unamuonya lakini anarudia tabia zilezile huenda ni ulevi kupindukia,wizi,kutumia pesa nyingi sana ndani ya muda mfupi,kutumia pesa zako bila kukupa taarifa, kutukana wazazi au ndugu zako mara kwa mara,kukuita majina ya aibu, haonyeshi ushirikiano wowote kwako,anakosa shukurani kwako, anakumbusha makosa ya zamani mara kwa mara, anachelewa kurudi nyumbani kwa makusudi mara kwa mara,anasikiliza sana maneno ya watu kutoka nje ,anakuwa na tabia tofauti tofauti kila siku,anakuwa na hasira kupita kiasi kwa vitu vidogo vidogo.


3.KUKUMBUKA MABAYA YAKE MENGI KULIKO MAZURI YAKE

Kama unakaa na kuvuta kumbukumbu za matukio mbalimbali yenye kuziumiza hisia zako unakuwa na orodha ndefu sana lakini huna kumbukumbu za mazuri yake.


Huna kumbukumbu lini alikwambia anakupenda,huna kumbukumbu za kukumbatiana,huna kumbukumbu za kushikwa mkono na kuongea nae kwa tabasamu usoni.


Zaidi kumbukumbu zako ni matukio kama kumfumania mara kwa mara,usaliti ,kutumia pesa zako nyingi sana bila kukupa taarifa, kusambaza taarifa za uongo na uzushi kila kona,kukuchafua kwa watu wa karibu,kuharibu mali zako,kuuza mali zako,kutishia kukuua au kukudhuru, kutukanwa,kufanywa kitu cha aibu,kukupiga, kukufokea, kuchelewa kurudi,kutoa ahadi hewa,huna kumbukumbu lini amekupa zawadi.

Ni kiashiria kwamba mahusiano yenu yanakwenda kuvunjika.


4.MAHUSIANO YENYE KUENDESHWA NA JUHUDI ZA MTU MMOJA

Kama mahusiano yako na mwenza wako unafanya kazi kubwa sana kuyaokoa ni wazi yapo njiani kuvunjika.

Utagundua hili kwa sababu unakuwa unampa ushauri kila siku namna ya kuendesha maisha yake,unataka kuingilia uhuru wake ili kuzuia asifanye makosa,unakuwa unajiweka karibu sana na ndugu zake ili wakupende lakini yeye hana mpango na ndugu zako,unakuwa na kiherehere mara kwa mara kutaka kumfurahisha lakini yeye hana mpango,unampa zawadi,unataka kumchukulia mkopo,unataka kumsaidia kukabiliana na matatizo yake yote lakini yeye kwako hafanyi hivyo, ghafla anakuwa mzigo kwako kila kitu anakutegemea wewe lakini yeye hana MSAADA wowote kwako.

Utajikuta ukipiga hesabu nini uapoteza endapo mkiachana huoni lakini huwezi kumuacha.

Utajikuta muda wote unakosa utulivu kama haonyeshi ushirikiano,utajikuta unamuona hana makosa wala mapungufu yoyote lakini wewe unajiona upo na makosa kila siku akiwa na hasira,akianza kununa,akikata mawasiliano unahisi chanzo ni wewe,akifanya makosa yeye unaomba msamaha wewe.


5.UNATUMIA FEDHA NYINGI SANA ILI KUMFURAHISHA

Kama unatumia pesa nyingi sana ili kumfurahisha mwenza wako lakini unabaki na hasira kupita kiasi,kinyongo,chuki, kisirisiri unaona mwenza wako amekuwa mzigo kwako.

Ni kiashiria cha mahusiano yenu yanakwenda kuvunjika.


Kama mwenza wako anaweza kutumia pesa zako nyingi sana bila kukupa taarifa wala haombi msamaha kwa kufanya hivyo zaidi anakuwa na hasira kupita kiasi,anakuwa mkali,anadai wewe ni mbinafsi kwa kukemea makosa yake ni kiashiria kwamba mahusiano yenu yanakwenda kuvunjika.




YAFUATAYO NI MÀUMIVU AMBAYO HUJITOKEZA BAADA YA MAHUSIANO KUVUNJIKA

Kama mahusiano yako na mwenza wako yamevunjika utaona mabadiliko yafuatayo mwilini

a.moyo kwenda mbio, kizunguzungu, kuchanganyikiwa, tumbo kuvurugika, kuumwa kichwa na mgongo, uchovu mwili mzima, kubanwa kifua, kutetemeka sana, miguu kuishiwa nguvu, kutokwa jasho bila joto, kuumia kooni,uchungu moyoni,hisia za kisasi,upweke kupita kiasi, kujichukia sana,kuanza kulia, kujifungia ndani kukwepa aibu na macho ya wengine.

b.Hofu ya kukosolewa, hofu ya kuachwa mpweke, hofu ya kitu kibaya kutokea ghafla, hofu ya kupata mshtuko wa moyo,hofu ya maisha Kuwa magumu sana,fikra kuvurugika,hisia za kudondoka ghafla,kushindwa kutuliza akili sehemu moja, kupoteza hisia kwenye vidole

c.Hofu ya kuonekana kituko, kupaniki ghafla, kuhisi unataka kufa ghafla, kichefuchefu, kukosa utulivu,huzuni kupita kiasi,kukata tamaa ya maisha,kuwa mkali kupita kiasi,kuanza kujitenga

d.kujilaumu , kujikosoa,kujuta sana, kujilaumu, kujichukia kupita kiasi,kukonda ghafla au kuongezeka uzito ghafla, kupoteza hamu ya kula au kula sana vyakula bila mpangilio,kukosa nguvu ya kutoka kitandani

e.kutamani kujiua,kuyachukia mapenzi, kupoteza hisia za mapenzi,hofu ya afya yako kuongezeka.


MADHARA YA MÀUMIVU MAKALI SANA MOYONI NI

Kama màumivu hayo yatazidi kuongezeka kwa kasi mwili wako utakuwa hatarini kupata magonjwa yafuatayo kisukari, madonda tumbo, uvimbe, shinikizo la damu, kupooza, kuugua mara kwa mara,

Changamoto zingine ni hedhi kuvurugika, ujauzito kuharibika,kifo cha ghafla au kujiua.

MAKOSA AMBAYO WATU WENGI HUFANYA MAHUSIANO YAKIVUNJIKA

a.Kupiga simu mfululizo, kutuma sms mfululizo,kutishia kujiua,kutishia kumdhalilisha mwenza wake wa zamani,kukata tamaa ya mapenzi

b.kutaka kujenga naye urafiki tabia hii husababisha upweke kupita kiasi kama haonyeshi ushirikiano wowote

c.Kuweka nyimbo za huzuni kwenye mitandao,kumpiga vijembe na mafumbo,kupost mwanamke au mwanaume mwengine ili kumfanya aone wivu

d.Kujisifia sana kwenye mitandao,kutaka kuonekana maisha yamekuwa mazuri sana baada ya mahusiano kuvunjika tabia hiyo huongeza upweke kupita kiasi na wivu kupita kiasi

e.Kuoa au kuolewa haraka sana ili kumkomoa mwanmke/ mwanaume matokeo yake usumbufu wa kuombwa msamaha na mwenza wa zamani huvunja mahusiano mazuri 

f.Kuendelea kufanya naye mawasiliano,kulipa kisasi, kujilaumu, kujitenga,kumchukia mwenza wako wa zamani,kutaka kurejesha mahusiano haraka.


UFUMBUZI WAKE

Kaa kimya muache huru usimuulize chochote, epuka kumsema vibaya, kumchafua mwenza wako wa zamani,kaa kimya bila mawasiliano yoyote kwa siku 30 mpaka 90 hayo màumivu yataondoka .

Epuka kutaka faraja yake au huruma yake,epuka kutaka aonekane mkosaji sana,epuka kutaka ajute,epuka kumpa vitisho kuwa maisha yake yatakuwa magumu bila wewe.

Kwa maelezo zaidi na ufafanuzi wa kilichoandikwa hapo juu unaweza kuwasiliana moja kwa moja na mwandishi. 

Imeandikwa na Mwanasaikolojia

Said Kasege +255 766 862 579

Temeke,Dar es salaam

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA