TCAA YATANGAZA KUTOUTAMBUA USAJILI CHUO CHA TANZANIA AVIATION COLLEGE CHENYE KAMPASI YA MWANZA, DAR ES SALAAM NA ARUSHA
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), inautangazia Umma kuwa haiutambui usajili wa chuo cha Tanzania Aviation College chenye kampasi katika mikoa ya Mwanza, Dar es Salaam na Arusha.
Chuo hiki kimekuwa kikitumia usajili namba CAA/ATO/050 ulioisha muda wake mwaka 2018. Kitendo hiki ni kinyume cha taratibu za usajili kama ulivyoainishwa katika Sheria ya Usafiri wa Anga, Sura ya 80 na Kanuni zake, The Civil Aviation (Approved Training Organisation) Regulations, 2017.
Baada ya Mamlaka kujiridhisha kuwa chuo tajwa hakijakidhi vigezo na hakitambuliki, TCAA inatoa wito kwa wazazi na wanafunzi wanaotaka kusoma kozi za Usafiri wa Anga kujiridhisha kwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga ili kupata uhakika kuhusu uhalali wa vyuo vinavyotambulika, orodha yake inapatikana katika tovuti ya Mamlaka.
Hivyo mafunzo ya usafiri wa anga yanayoendeshwa na chuo hiki kwa mgongo wa kutambulika na TCAA ni kinyume na sheria lakini pia, wahitimu wa chuo hiki wanakosa sifa za kupata leseni kutoka TCAA hivyo kushindwa kupata ajira.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imesema haiutambui usajili wa Chuo cha Tanzania Aviation College kinachotoa mafunzo ya usafiri wa Anga chenye kampasi zake mikoa Mwanza, Dar es salaam na Arusha kwa kukiuka taratibu za uendeshaji wa Vyuo vya usafiri wa anga.
Hatua hiyo imekuja mara baada Mamlaka ya usafiri wa anga Tanzania (TCAA) kufanya ukaguzi katika Chuo hicho Kampasi ya Mwanza na kujiridhisha kuwa kimekuwa kikitumia usajili namba CAA/ATO/050 ulioisha muda wake tangu mwaka 2018, ambapo kitendo hicho ni kinyume cha taratibu za usajili kama ulivyoainishwa katika Sheria ya Usafiri wa Anga, sura ya 80 na Kanuni zake.
Baada va Mamlaka kujiridhisha kuwa chuo tajwa hakijakidhi vigezo na hakitambuliki, hivyo mafunzo ya usafiri wa anga yanaendeshwa chuoni hapo kwa mgongo wa kutambulika na TCAA ni tendo ambacho ni kinyume na sheria lakini pia, Wahitimu wa Chuo hicho wanakosa sifa za kupata leseni kutoka TCAA hivyo kushindwa kupata ajira.
Itakumbukwa sep 30, 2020 Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ilikifungia Chuo hicho kutokana kukiuka taratibu za usajili lakini uongozi wa chuo hiki uliendelea kutoa mafunzo haya kinyemela.
Wakati Mkuu wa Chuo hiki akijitetea kuwa wahitimu wake hawata hitaji leseni kutoka TCAA, Wanafunzi pamoja na Mwalimu wa Kozi hizo wamedai kuwa wanahitaji kupata leseni kutoka TCAA ili waweze kutambulika katika utendaji wao.
0 comments:
Post a Comment