KAIMU KURUGENZI MKUU TCAA ATOA ELIMU MAONESHO YA MIAKA 61 YA MAPINDUZI ZANZIBAR
Mnamo Januari 6, 2025, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bi. Flora Alphonce, alitembelea banda la TCAA katika maonesho ya maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Nyamanzi kuanzia Januari 1 hadi 15, 2025.
Akiwa katika banda hilo, Bi. Flora aliungana na timu ya maonesho kutoa elimu kwa wananchi waliofika kujifunza na kupata taarifa kuhusu sekta ya usafiri wa anga nchini.
Bi. Flora alisisitiza dhamira ya TCAA katika kutoa huduma bora kwenye sekta ya usafiri wa anga, akisema, "TCAA imejidhatiti kuhakikisha inatoa huduma bora na salama katika sekta ya usafiri wa anga nchini, ili kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii."
Maonesho haya yanatoa fursa kwa wananchi kuelewa zaidi kuhusu shughuli na huduma zinazotolewa na TCAA, pamoja na mchango wake katika kuhakikisha usalama na ufanisi wa usafiri wa anga nchini.
0 comments:
Post a Comment