Showing posts with label usalama. Show all posts
Showing posts with label usalama. Show all posts

Wednesday, 7 June 2017

IGP SIRRO AFANYA ZIARANA KUKUTANA NA WAZEE KIBITI NA RUFIJI, ATANGAZA MSAKO MKALI

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro  jana alifanya mazungumzo na wazee pamoja na viongozi wa dini wilayani Kibiti mkoani Pwani ili kubaini waalifu wanaotekeleza mauaji ya watu wilayani humo na kusema vyovyote itakavyokuwa lazima watawarudisha kwenye msitari.

IGP Sirro alisema kupitia mazungumzo hayo tayari amepata taarifa za wahalifu hao ingawa ni mapema kuziweka wazi ila amewakikishia wananchi kuwa waalifu wao ni lazima watapatikana.

“Kubwa ni kwamba wazee wetu wa Kibiti wametueleza taarifa nyingi sana na mnavyojua hawa waalifu wanaishi ndani ya Kibiti, ndani ya Ikwiriri, kwa hiyo wazee wetu wamejaribu kutueleza ni wapi tunaweza kuwapata na chanzo cha mambo yote haya,” alisema IGP Sirro na kuongeza;

“Kwa hiyo kimsingi mambo mengine mengi ni ya kipelelezi ambayo siwezi kuyasema kwa sasa, lakini kikubwa wametupa dira, muelekeo kwa maana kwamba wale ndugu zetu au maadui zetu kwa lugha nyepesi tumepata njia nzuri ya kudeal nao. Kwa hiyo nitume salamu kwao kwamba waendelee kukimbia lakini njia ya muongo ni fupi na mwisho wa siku tutawarudisha kwenye mstari"

Saturday, 7 January 2017

MAREKANI KUMSAKA MTOTO WA OSAMA BIN LADEN ALIYEAPA KULIPA KISASI

Marekani imesema kuwa imemuorodhesha mtoto  wa mwisho wa Osama Bin Laden, Hamza, katika orodha ya magaidi wanaosakwa na taifa hilo.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema kuwa Hamza Bin Laden ameanza kushiriki katika maswala ya kundi la al Qaeda, kundi la jihad lililofadhiliwa na babake.

Hamza amesema kuwa atalipiza kisasi mauaji ya babake yaliotekelezwa na kikosi maalum cha Marekani kwa kutekeleza mashambulizi dhidi ya Wamarekani.

Hamza amepigwa marufuku  kufanya biashara na raia wa Marekani huku mali zake zikizuiliwa pia.

Mamake Hamza ni Khairiah Sabar, mmoja wa wake za Osama aliyekamatwa wakati wa shambulio la wanajeshi wa Marekani kwenye maficho ya Osama mjini Abbotabad nchini Pakistan mwaka 2011.

Mkuu wa kitengo cha usalama cha kundi la al-Qaeda Ibrahim al-Banna pia ameongezwa katika orodha hiyo .

Marekani imetoa kitita cha dola milioni 5 kwa mtu yeyote atakayemkamata al-Banna.

Hamza bin Laden alitambuliwa kuwa mmoja wa viongozi wa al-Qaeda mwaka 2015 na baadaye akaapa kulipiza kisasi mauaji ya babake mwezi Julai mwaka uliopita.
 
Katika ujumbe wa sauti wa dakika 21 wenye kichwa "We Are All Osama," (Sote ni Osama), na uliochapishwa katika mitandao, aliapa lazima angelipiza kisasi mauaji ya babake mwaka 2011 nchini Pakistan.

''Tutaendelea kuwasaka na kuwapiga popote pale mtakapokuwa mmejificha ati nyuma ya pazia za usalama kwa maovu mnayoyaendeleza ,Palestina, Afghanistan, Syria, Iraq, Yemen, Somalia na kote kwenye ardhi ya waislamu mnayokalia,'' shirika la habari la Reuters lilimnukuu.

''Na kwa wale wanaodhania kuwa tutakuwa tukilipiza kisasi mauaji ya Osama ole wenu, kwanini sisi tutakuwa tukilinda dini ya kiislamu''alisema Hamza.

Hamza, kulingana na wachanganuzi, alitambulishwa na kiongozi wa kidini wa kundi la al-Qaeda Ayman al-Zawahiri katika ujumbe huo uliolenga kuwavutia vijana ambao kwa sasa wamejiunga kwa wingi na kundi la Islamic state.

Hamza sasa anaungana na nduguye wa kambo, Saad, kuwa miongoni mwa watu wa jamii ya Osama walioorodheshwa kuwa magaidi.

Chanzo: BBC

Tuesday, 9 February 2016

ZIJUE AINA TANO ZA MITUNGI YA KUZIMIA MOTO


Na Sek  David
1.MTUNGI WA MAJI(WATER)
Mtungi huu una rangi NYEKUNDU wote. Mtungi huu hautumiki kuzimia moto wa umeme au mafuta, ila unazima aina nyingine zote za moto. Mtungi huu ni hatari sana kuutumia kwenye moto wa umeme
2. MTUNGI WA KABONDAYOKSAIDI(CO2)
Mtungi huu hutumika kuzima aina nyingi za moto ukiwamo umeme. Ni mwekundu lakini una lebo NYEUSI kama kitambulisho chake. Wakati wa kuzima moto usishike mwishoni mwa bomba kwakuwa gesi inayotoka ni ya baridi sana unaweza kuganda.
3. MTUNGI WA POVU(FOAM) Mtungi huu una rangi ya KRIMU kama kitambulisho chake. kwingine kote ni mwekundu. Unazima moto wa vitu vya majimaji pamoja na vitu vigumu 4. MTUNGI WA PODA(POWDER) Mtungi huu una lebo ya BLUU kama kitambulisho chake. Unaweza kuzima moto wa gesi, majimaji, na vitu vigumu.

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA