HII NDIO HALI ILIYOKUWA MOSHI KWENYE MGOMO WA MABASI MADOGO..ULIOISHA MUDA SIO MREFU..CHEKI HAPA
| Kituo kikuu cha mabasi yaendayo sehemu mbalimbali ndani ya mkoa wa Kilimanjaro na Arusha ikiwa haina gari baada ya wamiliki wa magari yaendyo maeneo hayo kugoma kutoa huduma. |
| Kutokana na mgomo huo ndipo madereva wa magari hayo na makondakta wakaamua kugeuza stendi hiyo uwanja wa mpira wa miguu likapigwa mbungi kati ya madereva na makondakta. |
| Ndipo askari walipoamua kuingilia kati na kuzuia mchezo huo uliokuwa hauna waamuzi wala milingoti ya kufunga magoli. |
| Ulinzi ukaimarishwa zaidi. |
| Baadhi ya makondakta na madereva wa magari hayo wakatiwa mikononi. |
| Hata hivyo hatua ya kukamatwa kwa madereva na makundakta kiliwatia hasira wapiga debe wakaamua kulipopoa gari la polisi kwa mawe na kuvunja kioo cha nyuma kama inavyoonekana hapa. |
| Abiria walilazimika kupanda gari la kusafirisha magazeti. |

0 comments:
Post a Comment