Saturday 22 March 2014

Maandamano Algeria kumpinga Bouteflika

Rais Bouteflika
Maelfu ya raia wa upinzani nchini Algeria wamehudhuria mkutano mkubwa wa hadhara katika mji mkuu wa Algiers ili kutaka watu wasusie uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi ujao.
Vyama vya upinzani vikiwemo vile vya dini vimepinga harakati za rais Abdelaziz Bouteflika kutaka kuliongoza taifa hilo kwa muhula mwingine wa miaka minne.
Wanasema kuwa hafai kuliongoza taifa hilo baada ya ugonjwa wa kupooza kumuathiri vibaya mwaka uliopita.
Maandamano kumpinga Rais Bouteflika
Mkutano huo ulifanyika ndani ya ukumbi wa michezo ambapo watu 5000 walikusanyika wakilaani harakati za Bouteflika kutaka kugombea urais kwa muhula wa nne.
Wanataka mageuzi ya sheria pamoja na kuishinikiza serikali kuangamiza ufisadi.
Bwana Bouteflika ambaye ana umri wa miaka 77 amekuwa haonekani hadharani miezi ya hivi karibuni,lakini waandishi wanasema kuwa ushawishi alionao katika chama tawala, jeshi na miongoni mwa wafanyibiashara huenda ukamsaidia kuchaguliwa kwa muhula mwingine.
Amekuwa mamlakani tangu mwaka 1999 na alifutilia mbali sheria za katiba mwaka 2008 ambazo zilimruhusu tu kuwa mamlakani kwa mihula miwili.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA