Saturday 22 March 2014

Papa Francis awaasa 'Mafia' kutubu



Photo: Papa Francis awaasa 'Mafia' kutubu   http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/03/140322_papa_mafia.shtml
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis.


Mkuu wa Mafia Italia Salvatore Riina
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amewaonya wanachama wa genge la Mafia kwamba watakwenda motoni iwapo hawatatubu dhambi zao.


Akizungumza katika sherehe ya maombi ya ndugu na jamaa za waathiriwa wa genge hilo waliouawa nchini Italia,Papa Francis amesema kuwa wanachama wa kundi hilo hawawezi kutumia fedha wanazopata kwenda peponi.
Wakati wa ibada hiyo majina ya watu 800 waliouawa na wanachama wa genge hilo yalisomwa.
Waandishi wanasema kuwa lengo la ibada hiyo ilikuwa kuonyesha kwamba kanisa katoliki linapinga uhalifu mbali na kujitenga na wakuu wa genge hilo wanaodai kuwa wafuasi wakubwa wa kanisa hilo.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA