Tuesday 25 March 2014

MAREKANI YAPELEKA KIKOSI MAARUMU CHA KUSAIDIA KUMSAKA KONY

98d84083-fb54-4b10-8c66-f.jpg Marekani inapeleka wanajeshi zaidi ya mara mbili ya kikosi cha operesheni maalum kusaidia kumtafuta mbabe wa vita Joseph Kony. Rais Barack Obama aliamuru kiasi cha wanajeshi 150 na angalau ndege nne za CV-22 kuelekea Uganda siku ya Jumapili ambapo ni mara ya kwanza kwa Marekani kupeleka ndege za kijeshi kumtafuta Kony na wapiganaji wake. Msako unalenga kwenye misitu inayopakana na Jamhuri ya Afrika ya kati, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC. Bwana Obama awali alipeleka kiasi cha wanajeshi 100 wa kikosi maalumu cha Marekani kuelekea kwenye eneo hilo mwaka 2011 ambako wamekuwa wakiwasaidia wanajeshi 5,000 wa kikosi cha operesheni za kieneo wa Umoja wa Afrika.
Pentagon inasema wanajeshi wa Marekani wana jukumu la kutoa taarifa na msaada na wanatumia silaha kwa kujilinda. Kony anatafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC kwa makosa 33 ya uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya binadamu. Aliendesha vita vikali vya msituni dhidi ya serikali la Uganda kwa takribani miongo miwili kabla ya kukimbia na wapiganaji wake kuelekea kwenye misitu ya Afrika ya kati katika mwaka 2005. Kony anaaminika kuwa na wapiganaji wachache waliobaki nae.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA