Mkuu wa Jeshi ajiuzulu Misri
Mkuu wa majeshi na waziri wa ulinzi Misri, Abdul Fattah al-Sisi, ametangaza kujiuzulu jeshini ili kugombea katika uchaguzi wa urais mwezi ujao. Wagombezi wote wanapswa kuwa raia.
Akizungumza Kwenye hotuba ya Televisheni huku akiwa amevalia sare ya kijeshi Abdel Fattah El Sissi amesema yeye sio mwanajeshi tena baada ya miaka 44 na kwamba amechukua hatua hiyo ili aweze kutimiza jukumu lingine muhimu.
Ni Bayana kwana Sisi hatakua na kibarua kigumu kujipatia ushindi katika uchaguzi wa Urais. Anaungwa mkono na idadi kubwa ya raia wa Misri na hadi sasa hana ushindani wowote.
Baadhi ya waliotaka kugombea urais wamejiondoa wakidai kwamba hawataweza kukampeni kwa njia huru.
Wafuasi wake Sisi wanamuona kama kiongozi imara ambaye anaweza kurejesha amani na udhabiti nchini Misri baada ya miaka mingi ya machafuko.
Wakosoaji wake wanasema ana msimamo mkali na amechangia pakubwa katika kusambaratisha na kuhujumu upinzani nchini Misri.
Mkuu huyo wa jeshi atakabiliwa na majukumu mazito ya kufufua uchumi uliofifia , kupambana na uasi na kuileta pamoja nchi iliyogawanyika. Ameahidi kutekeleza mabadiliko makubwa lakini akaonya kuwa hawezi kufanya miujiza.
0 comments:
Post a Comment