WAZIRI ALIPOWAPIGA MARUFUKU WANANCHI KULA POPO
Mnyama aina ya popo wameonekana kuwa chanzo kikuu kinachosababishwa kuibuka kwa virusi vya Ebola nchini Guinea.
Waziri wa Afya wa Guinea amekataza kuuzwa na kutumiwa kwa popo ili kuzuia kusambaa wa ugonjwa unaoua wa virusi vya Ebola.
“Popo wameonekana kuwa ndio chanzo kikuu kwa mlipuko wa ugonjwa huu wa Ebola hasa katika maeneo ya vijiji vya kusini”, alisema Rene Lamah
Watu 62 wameshafariki kutokana na virusi vya Ebola nchini Guinea, huku kesi kadhaa zikiripotiwa nchi za jirani za Liberia na Sierra Leone. Ebola husambazwa kwa mahusiano ya karibu na huua waathiriwa kati ya asilimia 25 na 90. Hakua kinga wala tiba iliyogunduliwa.Dalili zake ni pamoja na kutokwa damu nje na ndani, kuharisha na kutapika
0 comments:
Post a Comment