ADEBAYOR APIGA MBILI ,SPURS IKIIKANDAMIZA SUNDERLAND 5-1,
Mpira kambani: Mlinda mlango wa Sunderland Vito Mannone (kulia) akiushangaa mpira uliozamishwa nyavuni na Adebayor
Heshima: Kocha wa SpursTim Sherwood (kulia) akimpigia saluti Adebayor baada ya kufunga bao la pili.
TOTTENHAM imeishushia kipigo kizito cha mabao 5-1 klabu ya Sunderland katika mchezo wa ligi kuu soka nchini England usiku huu.
Kocha mkuu wa Spurs, Tim Sherwood amebaki ameduwaa baada ya vijana wake kuonesha soka safi wakati yeye yuko mbioni kuondolewa katika wadhifa huo.
Spurs tayari wameshatangaza kuwa mwishoni mwa msimu Sherwood hataendelea kuwa kocha mkuu, badala yake wanamhitaji Van Gaal ambaye ni kocha wa timu ya Taifa ya Uholanzi.
Mabosi wa Spurs wanataka kukifanyia maboresho makubwa kikosi chao majira ya kiangazi mwaka huu.
Shukurani zimwendee mshambuliaji raia wa Togo, Emmanuel Adebayor aliyefunga mabao mawili, huku mengine yakitiwa kambani na Harry Kane, Christian Eriksen na Gylfi Sigurdsson.
Baada ya matokeo ya mechi zote wikiendi iliyopita na leo usiku, timu kumi bora katika msimamo hizi hapa chini;
LIVERPOOL--74
CHELSEA--72
MANCHESTER CITY--70
ARSENAL--64
0 comments:
Post a Comment