RAIS WA CHINA AZURU ZIMBABWE
Xi Jinping akitumbuizwa nchini Zimbabwe
Rais wa China Xi Jinping yuko nchini Zimbabwe katika ziara ya siku mbili inayolenga kujenga mahusiano na Zimbabwe.
Rais huyo anatarajiwa kufanya mkutano wa moja kwa moja na mwenyeji wake hii leo rais Robert Mugabe.
Jinping ndiye rais wa kwanza wa China kufanya ziara nchini Zimbabwe katika kipindi cha takriban miaka 20
Xi akikagua gwaride la heshima Zimbabwe
Rais huyo
wa China amepokelewa kwa shangwe na taadhima katika uwanja wa ndege wa
kimataifa na raia waliojawa na furaha wakiongozwa na rais Mugabe.
Maafisa
nchini Zimbabwe wanatarajia kuwa makubaliano kadha yenye thamani ya
mabilioni ya pesa yatatiwa sahihi yakiwemo mikataba ya ujenzi wa miundo
msingi, kilimo na vilevile katika sekta ya uchukuzi.
Maafisa nchini Zimbabwe wanatarajia kuwa makubaliano kadha yenye thamani ya mabilioni ya pesa
Lakini
wanasiasa wa upinzani wamepuuzilia mbali ziara hiyo wakisema kuwa
Uchina, haitawekeza hadi chama tawala cha ZANU-PF kiamue ni nani mrithi
wa Mugabe ambaye sasa ana umri wa miaka tisini na moja.
Uwekezaji
wa China barani Afrika ulidorora kwa zaidi ya asilimia 40 miezi sita ya
kwanza ya mwaka huu kutokana ukuaji mdogo wa uchumi nchini humo.-BBC
0 comments:
Post a Comment