Wednesday 16 April 2014

ARSENAL YAFUFUA MATUMAINI YA KUCHEZA UEFA MSIMU UJAO, YAILAZA WEST HAM 3-1



MATUMAINI ya Asernal kufuzu kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao yameanza kufufuka baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya West Ham kwenye mchezo wa ligi kuu soka nchini England uwanja wa Emirates.
Lukas Podolski amefunga mabao mawili  katika dakika ya 44 na 78, huku  moja likifungwa na Olvier Giroud dakika ya 54.
Westham walikuwa wa kwanza kufunga leo hii katika dakika ya 40 kipindi cha kwanza kupitia kwa Matthew Jarvis .
Mashabiki wa Asernal huwa hawana imani kubwa na Giroud na katika mchezo wa leo alikosa nafasi kadhaa kipindi cha kwanza, lakini wakati mashabiki wakijiuliza kama mshambuliaji huyo anaweza kuwa tegemeo kwa siku za usoni, alifunga bao muhimu mno katika ushindi huo.
Umuhimu wa bao la Giroud unatokana na uhitaji mkubwa wa Asernal kufuzu michuano ya UEFA msimu ujao.
Kikosi hicho cha Aserne Wenger kilianza vizuri ligi na kuongoza kwa muda mrefu, lakini mambo yakabadilika ghafla na kuwapisha wanaume Chelsea, Man City na Liverpool ambao wanachuana mpaka sasa.
Sasa Wenger na vijana wake wapo katika hatari ya kushindwa kufuzu UEFA kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 17 baada ya kuwapisha Everton katika nafasi ya nne kwa muda.
Lakini baada ya kushinda mechi ya leo dhidi ya wapinzani wao wa London, Asernal wamerejea nafasi ya nne kwa kufikisha pointi 67, huku Everton wakishuka mpaka nafasi ya tano kwa pointi zao 66, lakini kesho wanacheza dhidi ya Crystal Palace.
Asernal Wenger baada ya mchezo amesema kuwa walikuwa katika presha kubwa ya kushinda mchezo, lakini ilikuwa mechi ngumu mno.
“Niliridhishwa na ukomavu wa timu yangu. Walionesha kutulia baada ya kufungwa bao la kwanza”.

“Kazi kubwa ilikuwa kusawazisha bao kabla ya mapumziko. Ilikuwa vita kubwa na ilikuwa ya kufurahisha”. Alisema Wenger.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA