Tuesday, 8 April 2014

MANUARI YA AUSTRALIA YANASA ISHARA ZA NDEGE ILIYOPOTEA YA MH370

Meli ya Australia Ocean Shield iliyonasa ishara mpya
Maafisa nchini Australia wanaongoza shughuli ya kuitafuta ndege ya Malaysia iliotoweka wamesema kuwa manuari moja ya wanamaji ya Australia imepata ishara zinazofanana na zilezinazotoka katika kijisanduku cheusi cha ndege chenye uwezo wa kurekodi.
Ishara hiyo imesikika katika kina cha takriban mita 4500 ndani ya bahari Hindi kupitia kwa chombo maalum kinachokokotwa na meli ya Ocean Shield 
Ishara hiyo ilinaswa na kurekodiwa kwa takriba Masaa mawili unusu kabla ya kutoweka.
Ramani ya eneo inakotafutwa ndege ya Malaysia MH370
Afisa mkuu, Angus Houston amesema kuwa ni dalili nzuri zaidi kwao tangia shughuli ya kuitafuta ndege hiyo ianze.
Amesema kuwa Ishara hizo zilinaswa na meli moja kusini mwa bahari hindi yapata kilomita 1000 kutoka pwani ya Australia.
Lakini amesema kuwa uthibtisho kwamba ishara hizo zinatoka katika ndege hiyo ya Mh370 utachukua siku kadhaa kubainika.
Manuari nyengine ya Uchina Ilikuwa imeripoti kunasa ishara jumamosi iliyopita kutoka eneo tofauti ya Bahari Hindi.
Haixun 01 ya China Ilikuwa ya kwanza kunasa ishara.
Manuari hiyo Haixun 01, inasemekana ilikuwa ikitumia kifaa aina ya SoNar kunasa ishara hiyo iiliyodaiwa kuwa inarusha mawasiliano kupitia mitabendi 37.5 sawa na ndege kama iliyotoweka.
Madai hayo hayajadhibitishwa kufikia sasa japo meli ya kijeshi ya Uingereza HMS Echo, imeelekea katika eneo hilo kutathmini chanzo cha ishara hiyo.
Kifaa cha kukokotwa cha kunasa ishara
Mwandishi wa BBC mjini Perth baada ya usakaji wa ndege kwa takriban mwezi mmoja sasa huenda shughuli hiyo ikafanikiwa.
Utafutaji huo unakabiliwa na tishio la kupitwa na wakati kwa kuwa battery ya rekoda ya ndege hiyo huenda ikaisha nguvu wakati wowote.
Rekoda hiyo inauwezo wa kutuma ishara kwa takriban siku thelathini.
Ndege hiyo ya Malaysia ilitoweka March tarehe 8 ikiwa inaelekea Beijing Uchina ikiwa na abiria 239.
Kufikia sasa hakuna mabaki yeyote ya ndege hiyo yaliopatikana.
Chanzo: BBC

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA