Tuesday, 8 April 2014

Mtu mmoja amefariki na wengine 19 wamejeruhiwa na majambazi eneo la Doma Morogoro


Mtu mmoja amefariki dunia na 19 wamejeruhiwa na kuporwa vitu mbalimbali zikiwemo simu za mkononi na fedha  baada ya majambazi kufunga barabara kwa mawe na magogo  na kisha  kuteka magari katika eneo la mkata doma barabara ya morogoro iringa.
Kwa mujibu wa kaimu kamanda polisi mkoa wa Morogoro John Laswai amesema tukio hilo limetokea majira ya usiku ambapo  majambazi hao wakiwa na silaha mbalimbali waliteka magari na kujeruhi abiria ambapo aliefariki dunia amefahamika kwa jina la Richard Mgombea ambaye alifariki wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Morogoro na magari ya magazeti ya kampuni ya Mwananchi limetumbukia mtoni wakati wakijaribu kukimbia majambazi hao. Nao majeruhi waliolazwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro wakielezea tukio hilo wamesema wao ni madareva wa magari ya it na   walikua wakitokea Mbeya kurudi Dar es salaam  wakikutana na foleni kubwa barabarani ndipo wakatekwa na kujeruhiwa ambapo wamekiri kupoteza fedha mali na simu za mkononi.
Nae mganga wa zamu katika hospitali ya mkoa wa Morogoro Dr Erick Rwegoshora amekiri  kuwepo  kwa taarifa za kifo na wamepokea majeruhi wengine wamelazwa na  wengine walitibiwa na kuruhusiwa .

CHANZO: ITV

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA